Mshubiri

(Elekezwa kutoka Aloe vera)

Kwa kipimo chenye jina la karibu angalia hapa shubiri

Mshubiri
(Aloe spp.)
Mlalangao (Aloe lateritia)
Mlalangao (Aloe lateritia)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
Oda: Asparagales (Mimea kama asparaga)
Familia: Xanthorrhoeaceae (Mimea iliyo na mnasaba na miti-nyasi)
Nusufamilia: Asphodeloideae (Mimea inayofanana na mshubiri)
Jenasi: Aloe
Ngazi za chini

Spishi ±450:
Angalia matini na Orodha ya spishi za Aloe

Mshubiri au msubili ni jina la mimea ya jenasi Aloe katika nusufamilia Asphodeloideae ya familia Xanthorrhoeaceae ambayo ni aina za sukulenti. Watu wengi wanaendelea kuweka Aloe ndani ya familia yake Aloaceae. Spishi kadhaa ni miti, lakini siku hizi huainishwa katika jenasi Aloidendron.

Majani ya mishubiri na dawa zilizotengenezwa kutoka haya huitwa shubiri.

Mimea hii ina shina fupi au haina shina kabisa, isipokuwa spishi zilizo miti. Majani ni marefu na manono na yanatoka shina karibu na wenziwe; yana miiba kingoni mwao. Maua yana umbo wa mrija mfupi na rangi yake ni nyekundu, pinki, ya machungwa, njano au nyeupe. Yapo mwishoni mwa kikonyo chenye vitawi au bila vitawi. Utomvu utokao mwenye majani hutumika kutengeneza dawa.

Spishi moja inajulikana sana: mshubirimani (Aloe vera), ambao unapandwa sana duniani na hutumika kwa kutengeneza dawa za uganga au za mitishamba.

Spishi nyingine inayopandwa sana katika Afrika na nchi nyingine za Tropiki ni mshubiri mwekundu (A. ferox).

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mshubiri kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.