Alofi ni mji mkuu wa nchi ya kisiwani cha Niue katika bahari ya Pasifiki.
Alofi ina wakazi 614 (2001). Kuna vijiji viwili vya Alofi North (wakazi 256) na Alofi South penye majengo ya serikali (wakazi 358).
Alofi iko kwenye pwani ya magharibi ya kisiwa, kando ya hori ya Alofi.