Alvin Wyatt
Mchezaji wa mpira wa miguu wa Amerika na mkufunzi wa michezo (aliyezaliwa 1947)
Alvin B. Wyatt (alizaliwa Desemba 13, 1947) ni mchezaji wa zamani wa Futiboli ya Marekani na kocha wa Futiboli na mpira wa kikapu. Alicheza kama mlinzi wa nyuma katika ligi ya NFL na timu za Oakland Raiders, Buffalo Bills na Houston Oilers pamoja na ligi ya WFL na timu ya Jacksonville Sharks. Wyatt alihudumu kama kocha mkuu wa Futiboli katika Chuo Kikuu cha Bethune–Cookman kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2009 na Chuo cha Edward Waters kutoka mwaka 2013 hadi mwaka 2017, akikusanya rekodi ya ukocha wa Futiboli ya vyuo vikuu ushindi 100–92. Pia alikuwa kocha mkuu wa timu ya mpira wa kikapu ya wanawake katika Bethune–Cookman kutoka mwaka 1978 hadi mwaka 1996, akiwa na rekodi ya ushindi 245–201.