Amato wa Sion (pia: Amat, Amé, Aimé; alifariki Breuil-sur-le-Lys, karibu na Amiens, Ufaransa, 690 hivi) alikuwa mmonaki Mkolumbani, halafu askofu wa mji huo, leo nchini Uswisi kuanzia mwaka 669, lakini baada ya miaka 5 ya uongozi bora alipelekwa uhamishoni na mfalme Theodoriki III[1][2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Septemba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.