Amina Afzali
Amena Safi Afzali (alizaliwa Herat, Afghanistan, 1957[1]) ni mwanasiasa nchini Afghanistan, ambaye alikuwa Waziri wa Kazi, Masuala ya Kijamii, Mashahidi, na Watu Wenye Ulemavu mnamo Januari 2010 baada ya kupata kura ya imani ya Bunge la Kitaifa la Afghanistan. Awali alihudumu kama kamishna wa Tume huru ya Haki za Binadamu hadi mwaka 2004 na kama Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana hadi ilipounganishwa na Wizara ya Habari na Utamaduni.
Maisha
haririAmena Safi Afzali alimaliza elimu yake ya juu katika masuala ya sayansi ya Chuo Kikuu cha Kabul mwaka wa 1978.[2] Alikuwa mwanzilishi wa Vituo vya Elimu na Mafunzo kwa wanawake, na shule ya kwanza ya bure jijini Kabul mnamo mwaka 1994. Machapisho kama 'Rahrawan Samia', 'Al-Momenat','Paiwand', na 'Mama' yalikuwa yameanzishwa na kuchapishwa chini ya uangalizi wake. Pia alihudumu kama kamishna wa Tume huru ya Haki za Binadamu hadi mnamo mwaka 2004. Ni mwanachama wa Idara ya Msingi ya Kitamaduni ya Jamee.[3]
Marejeo
hariri- ↑ "H.E. Amina Afzali Profile 1". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-03. Iliwekwa mnamo 2013-08-20.
- ↑ "Undani wa Amina Afzali". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-03. Iliwekwa mnamo 2013-08-20.
- ↑ "Kazi za Awali". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-03. Iliwekwa mnamo 2013-08-20.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amina Afzali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |