Amiri au Emir (ar. ‏امير‎ amīr au tur. emir) ni cheo cha mtawala mwislamu anayesimamia emirati. Kiasili maana yake ni "mwenye amri" kama cheo cha kijeshi au kiserikali.

Amiri Jabir al-Ahmad al-Jabir Al Sabah

Katika miaka ya kwanza ya Uislamu amiri alikuwa mkuu wa jeshi au sehemu ya jeshi. Baada ya kutwaa nchi alikuwa na nafasi kama gavana ya khalifa. Kutokana na upanuzi wa himaya ya kiislamu na ushaifu wa serikali kuu amiri aliweza kutawala mara nyingi kama mfalme mdogo lakini kwa kawaida alitafuta kibali cha khalifa.

Cheo cha kihistoria

hariri

Cheo hiki kilipatikana kwa maumbo mbalimbali kama

  • amir al-mu’minin („mkuu wa waumini“) ilikuwa cheo cha heshima kwa makhalifa tangu Umar. Hadi leo ni cheo kimoja cha sultani wa Moroko.
  • amir al-umara’ („amiri wa maamiri“) ilikuwa cheo cha jemadari mkuu wa jeshi la Waabasiya. Baadaye katika Milki ya Osmani ilikuwa cheo cha gavana wa jimbo kubwa.
  • amir al-bahr (‏امير البحر‎, „amiri wa bahari“) ilikuwa cheo cha kiongozi wa jeshi la maji ikaingia katika lugha za Kiulaya kama "admiral".

Cheo cha mtawala wa emirati

hariri

Nchi kadhaa zinazotumia jina "emirati" na cheo cha amiri kama mkuu wa dola ziko kwenye Bara Arabu. Mfano ni Kuwait na Qatar. Pia nchi zilinazojulikana kwa Kiswahili kama Falme za Kiarabu zinajiita emirati chini ya maamiri.

Amiri wa Bahrain alijiita mfalme tangu 2002.

Marejeo

hariri


  • WorldStatesmen Religious Organisations – see also many present Muslim countries