Sultan (kar. سلطان sultân:) ni cheo cha kiislamu cha mtawala wa nchi anayerithi nafasi yake kama mfalme.

Sultan Mehmed II Fatih wa Uturuki

Maana ya neno

hariri

Neno lenyewe lamaanisha "nguvu", "mamlaka" au "utawala" likawa baadaye kama cheo cha mtawala wa kiislamu mwenye kujitegemea bila kuwa na mwingine juu yake.

Masultani katika historia

hariri

Kiasili cheo cha Sultan ilikuwa ngazi moja chini ya Khalifa. Lakini watawala wa Milki ya Osmani waliendelea kujiita "sultani" hata baada ya kupokea cheo cha khalifa pia.

Baadaye cheo cha sultani kilitumiwa katika nch mbalimbali na watawala wa ngazi mbalimbali.

Katika historia ya Uswahilini "sultani" ilikuwa mara nyingi neno lingine kwa chifu mkubwa kama yeye alikuwa Mwislamu.

Katika historia sehemu ya watawala wa Kiislamu walipendelea cheo cha mfalme (kar.: malik) au Emir / Amir (mwenye amri).

Masultani leo

hariri

Leo hii kuna nchi mbili zinazotawaliwa na mfalme mwenye cheo cha Sultani ni Omani na Brunei.

Masultani wengine wenye madaraka ni watawala wa majimbo tisa ya shirikisho la Malaysia (Johor, Kedah, Kelantan, Pahang, Perak, Selangor na Terengganu).

Kuna watawala wa jadi katika nchi mbalimbali wanaoendelea kutumia cheo lakini hawana madaraka tena.

Watawala wa nchi Moroko (tangu 1956), Uarabuni wa Saudia, Yordani (tangu 1946) wanatumia cheo cha mfalme (malik). Nchi za Libya, Misri, Irak na Yemeni zilikuwa na wafalme.

Nchi kama Kuwait na falme za Kiarabu hutawaliwa na watawala wanaorithi cheo lakini wanatumia cheo cha "amiri".