Bahrain
Bahrain (kwa Kiarabu: مملكة البحرين Mamlakat al-Baḥrayn, Ufalme wa Bahrain) ni nchi ya visiwa na ufalme mdogo katika Ghuba ya Uajemi karibu na pwani ya Saudi Arabia.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Bahrainona | |||||
Wimbo wa taifa: بحريننا (Bahrainona) "Bahrain yetu" | |||||
Mji mkuu | Manama | ||||
Mji mkubwa nchini | Manama | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Hamad Bin Isa Al Khalifa Khalifah ibn Sulman Al Khalifah Salman Bin Hamad Al Khalifa | ||||
Uhuru tarehe |
15 Agosti 1971 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
786.5 km² (ya 173) 0 | ||||
Idadi ya watu - 2020 kadirio - 2010 sensa - Msongamano wa watu |
1,463,265a (ya 149) 1,234,571 1,912.7/km² (ya 3) | ||||
Fedha | Bahraini Dinar (BHD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+3) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .bh | ||||
Kodi ya simu | +973
- | ||||
a Includes 235,108 non-nationals (Julai 2005 estimate). |
Jiografia
haririBahrain iko upande wa mashariki wa Bara Arabu.
Eneo lake lina visiwa asilia 50 na vingine 33 vilivyotengenezwa na binadamu. Vikubwa kati ya hivyo ni:
- kisiwa kikuu cha Bahrain chenye urefu wa km 48 na upana wa km 16: kina 85% za eneo lote la ufalme na ni mahali pa mji mkuu Manama. Kimeunganishwa kwa daraja na:
- kisiwa cha Muharraq (chenye km² 18) penye uwanja wa ndege.
- funguvisiwa la Hawar (km² 50) karibu na pwani ya Qatar.
- kisiwa cha Umm Na'san (km² 19) kisicho na wakazi wa kudumu kwa sababu hakina maji; barabara inayounganisha Bahrain na Saudia kwa njia ya daraja inapita hapo.
- kisiwa cha Sitra (km² 10) kimeunganishwa pia kwa daraja na kisiwa kikuu; pana viwanda hapo.
Nchi ni tambarare; kilima cha juu ni Jabal ad-Dukhan chenye m 137 juu ya UB.
Sehemu kubwa ya eneo ni jangwa, lakini kaskazini mwa kisiwa kikuu pana visima na kilimo cha bustani na mitende.
Historia
haririBahrain ndiyo makao ya ustaarabu wa Dilmun. Ilipata umaarufu tangu zamani kwa kuvua lulu bora kuliko zote duniani hadi karne ya 19.
Bahrain ilikuwa kati ya maeneo ya kwanza kuongokea Uislamu, mwaka 628 BK.
Baada ya kipindi cha utawala wa Waarabu, Bahrain ilitekwa na Wareno mwaka 1521 hadi 1602 walipofukuzwa na Shah Abbas I wa nasaba ya Safavid chini ya Dola la Uajemi.
Mwaka 1783, ukoo wa Bani Utbah uliteka Bahrain kutoka kwa Nasr Al-Madhkur na tangu hapo nchi imetawaliwa na ukoo wa Al Khalifa, Ahmed al Fateh akiwa hakimu wa kwanza wa Bahrain.
Tangu mwaka 1820 Visiwa hivyo pamoja na Qatar na Falme za Kiarabu vilikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.
Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.
Wakazi
haririWakazi wengi (54%) ni wahamiaji kutoka nchi nyingi duniani, hasa India na nchi nyingine za Asia (43.4%), wakiwa na lugha na dini mbalimbali.
Wenyeji (46%) ni Waarabu, lakini pia Waajemi, Wabeluchi na Waafrika.
Lugha rasmi ni Kiarabu, lakini baadhi ya wenyeji na wahamiaji wengi wanatumia kwanza lugha nyingine. Kiingereza kina nafasi kubwa.
Upande wa dini, wengi (80.6%) ni Waislamu, ila upande wa madhehebu wamegawanyika kati ya Washia (65-75%) na Wasuni. Uislamu ndio dini rasmi. Wakristo wa madhehebu mbalimbali ni asilimia 12.1, wakiwemo wahamiaji wengi, lakini pia wenyeji. Wahindu ni 6.4% na Wabuddha 0.4%.
Uchumi
haririUchumi wa Bahrain hutegemea hasa mafuta ya petroli yanayozalisha 30% ya pato la taifa na 60% za mapato yote ya serikali.
Serikali imejitahidi kujenga matawi mengine ya uchumi hasa viwanda vinavyotumia mafuta kwa kutengeneza bidhaa za aina nyingi pamoja na biashara.
Kati ya nchi za Kiarabu ndiyo inayostawi kiuchumi haraka zaidi.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Tovuti ya serikali Ilihifadhiwa 25 Mei 2009 kwenye Wayback Machine.
- Official government portal
- Kingdom of Bahrain, Ministry of Foreign Affairs website
- Bahrain entry at The World Factbook
- Bahrain katika Open Directory Project
- Bahrain profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Bahrain
- Key Development Forecasts for Bahrain from International Futures
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahrain kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |