Amos Kimunya
Amos Muhinga Kimunya (alizaliwa 6 Machi 1962) ni mwanasiasa wa Kenya na Mbunge wa Jimbo la Kipipiri aliyepata kuwa Waziri wa Biashara. Pia alikuwa Waziri wa Fedha kutoka mwaka 2006 hadi Julai 2008, wakati alipojiuzulu kutokana na kashfa ya Hoteli ya Grand Regency. Hapo awali, alikuwa Waziri wa Ardhi na Makazi.
Maisha ya awali na elimu
haririKimunya alizaliwa Murang'a na mara moja alihamia Wilaya ya Nyandarua, Kenya.
Ana digrii ya Biashara (Uhasibu) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Yeye pia ana cheti cha Certified Public Accountant (CPA, K) na Certified Public Secretary (CPS, K). Awali alikuwa Mwenyekiti wa ICPAK ambalo ni mwili wa kitaifa wa Certified Public Accountants.
Wasifu wa kisiasa
haririWakati National Rainbow Coalition (NARC) ilishinda uchaguzi mkuu Desemba 2002, Rais Mwai Kibaki alimteua Kimunya kama Waziri wa Ardhi na Makazi. Alikuwa kuchaguliwa Mbunge wa Jimbo la Kipipiri. Tarehe 14 Februari 2006 aliteuliwa kama Waziri wa Fedha na Rais Kibaki kufuatia kujiuzulu kwa David Mwiraria, ambaye alikuwa amejiuzulu ili uchunguzi wa kashfa ya Anglo leasing uweze kuendelea.
Kimunya alibakia kama waziri wa Fedha katika Baraza la Mawaziri walioteuliwa na Kibaki on 8 Januari 2008, kufuatia utata wa Uchaguzi Mkuu wa 2007 [1] Baada ya ugawaji madaraka kati ya Kibaki na Raila Odinga, wote ambao alidai ushindi katika uchaguzi wa rais, Kimunya alibakia na kazi yake Bunge ilitotajwa tarehe 13 Aprili 2008.[2][3]
On 2 Julai 2008, Kimunya alipoteza kura ya kutokuwa na imani, ambayo ilikuwa imetokona na uuzaji wa Grand Regency Hotel. Ilidaiwa kuwa hoteli iliuzwa kwa thamani ndogo sana kulingana na thamani yake halisi, iliponunuliwa na kampuni kutoka Libya.[4] Katika utetezi wake, Kimunya alisema kuwa alikuwa na rekodi safi ya kupambana na rushwa.
Kimunya alijiuzulu kutoka katika baraza la mawaziri tarehe 8 Julai 2008 ili madai hayo yachunguzwe baada ya umma kutia mashinikizo makali ajiuzulu. Siku chache kabla ya kujiuzulu kwake, alikuwa ameapa kubakia katika kazi yake na kupambana na jaribio lolote la kushinikiza kujiuzulu kwake, alikwenda mbele na kutangaza kuwa "mimi ni afadhali nife kuliko kujiuzulu!" Kwa hiyo, kujiuzulu kwake kulikuja kama mshangao kwa wengi.
Tarehe 25 Novemba 2008, Uchunguzi rasmi ulimwondolea mashtaka yote. Ripoti ya tume haikutolewa kwa umma.[5]
Kimunya alirudishwa kwa Bunge na Rais Kibaki kama Waziri wa Biashara tarehe 23 Januari 2009. [6]
Tarehe 15 Agosti 2009 mlinzi wake alipigwa risasi na majambazi akiwa anaendesha gari Nairobi. Kimunya hakuwa pale.
Marejeo
hariri- ↑ "Kenya: Rais Kibaki achagua baraza la Mawaziri", The East African Standard (allAfrica.com), 8 Januari 2008.
- ↑ "Kenya yafichua mawaziri wa Serikali ya muungano", BBC News, 13 Aprili 2008.
- ↑ Anthony Kariuki, " Kibaki amtaja Raila kama Waziri Mkuu katika baraza jipya", nationmedia.com, 13 Aprili 2008.
- ↑ "Waziri ajiuzulu kutokana na kashfa ya hoteli", Al Jazeera, 8 Julai 2008.
- ↑ Kashfa ya Hoteli Kenya: Waziri wa Fedha kutohusika
- ↑ Waziri mkuu atangaza mpango mpya wa mawaziri Radio France International, 23 Januari 2009
Angalia Pia
haririViungo vya nje
hariri- http://www.parliament.go.ke/MPs/members_kimunya_m.php Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.