Amr Abd El-Basset Abd El-Azeez Diab (kwa Kiarabu: عمرو عبد الباسط عبد العزيز دياب; amezaliwa Port Said, Misri[1]11 Oktoba 1961) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Misri.

Amr Diab
عمرو دياب
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaAmr Abd El-Basset Abd El-Azeez Diab
Pia anajulikana kamaEl Hadaba الهضبة (The Plateau)
Amezaliwa11 Oktoba 1961 (1961-10-11) (umri 63)
ChimbukoPort Said, Msri
Kazi yakeMwimbaji], mtunzi wa melodi, mwigiaji
AlaSauti, gitaa, oud, piano
Miaka ya kazi1983–hadi sasa
StudioSawt El Delta (zamani)

Alam El Phan (zamani)

Rotana Records (zamani)

Nay For Media (sasa)
Wavutiwww.AmrDiab.net
Amr Diab akiwa na tuzo zake 7 za "World Music Awards".

Kulingana na mtafiti Michael Frishkopf, bwana huyu amebuni mtindo wake wa kipekee ulioitwa "Mediterranean Music", wenye mchanganyiko wa mdundo wa Kimagharibi na Kimisri.[2] Mwaka wa 1992, amekuwa msanii wa kwanza wa Kiarabu kuanza kutengeneza video zenye teknolojia ya hali ya juu.[2]

Maisha ya awali

hariri

Amr Diab alizaliwa mnamo tarehe 11 Oktoba 1961 mjini Port Said, Misri kutoka katika familia ya kisanii. Baba yake, Mzee Abdul Basset Diab, alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Mfereji wa Suez na alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya ujenzi iliyokuwa inajulikana kwa jina la Marine Construction & Shipbuilding huko Mfereji wa Suez. Baba yake mzazi alihusika vilivyo katika kutia utambi harakati za awali za kazi ya muziki ya Diab. Diab, katika umri wa miaka sita, alianza kupata umaarufu baada ya kuimba wimbo wa taifa la Misri "Bilady, Bilady, Bilady" katika kumbukizi za kila mwaka mnamo Julai 23 huko Port Said mbele ya hayati Gamal Abdel Nasser. Matokeo yake, akazawadia gitaa kutoka kwa gavana wa Port Said kipindi hiko, na kuanza kutambulika nchi nzima. Diab ni mhitimu wa shahada ya muziki wa Kiarabu kutoka katika Chuo Kikuu cha Sanaa cha Kairo ("Cairo Academy of Arts) mnamo mwaka wa 1986.[3][onesha uthibitisho]

Albamu

hariri

Video za muziki

hariri

Diab ni moja kati ya waimbaji wa kwanza kabisa kuchochea video za muziki katika ulimwengu wa Kiarabu na Mmisri wa kwanza kuonekana kwenye video.

Diskografia

hariri

Albamu rasmi

  • 1983: Ya Tareeq (يا طريق - O Road)
  • 1984: Ghanny Men Albak (غنّي من قلبك - Sing From Your Heart)
  • 1986: Hala Hala (هلا هلا - Welcome, Welcome)
  • 1987: Khalseen (خالصين - We're Even)
  • 1988: Mayyal (ميّال - In Love)
  • 1989: Shawaana (شوقنا - Missing You)
  • 1990: Matkhafeesh (متخافيش - Don't Worry)
  • 1991: Habiby (حبيبي - My Love)
  • 1992: Ayamna (أيامنا - Our Days)
  • 1992: Ice Cream Fi Gleam (أيس كريم في جليم - Ice Cream In Gleam)
  • 1993: Ya Omrena (يا عمرنا - Our Life)
  • 1994: W Ylomoony (و يلوموني - And They Blame Me)
  • 1995: Ragaeen (راجعين - We'll Be Back)
  • 1996: Nour El-Ain (نور العين - Light Of The Eye)
  • 1998: Awedoony (عوّدوني - They Got Me Used To)
  • 1999: Amarein (قمرين - Two Moons)
  • 2001: Aktar Wahed (أكتر واحد - The Most One)
  • 2003: Allem Alby (علم قلبي - Teach My Heart)
  • 2006: Zekrayat (ذكريات - Memories)
  • 2009: Wayah (ويّاه - With Him)
  • 2010: Aslaha Btefre' (اصلها بتفرق - Because She Makes A Difference)
  • 2011: Banadeek Ta'ala (بناديك تعالى - I'm calling you, come )
  • 2013: El Leila (الليلة - Tonight)
  • 2014: Shoft El Ayaam (شفت الأيام - Seen The Days)
  • 2016: Ahla w Ahla (أحلي و أحلي - More & More Beautiful)
  • 2016: Mn Asmaa Allah Al Hosna
  • 2017: Maadi El Nas

Albamu Zisizo Rasmi

  • 1984: Forsan Asia ( Asia Horsemen - فرسان آسيا )
  • 1986: Menin Ageeb Nas (Where Can I Get People - منين أجيب ناس ) – ( Yanabee' El Nahr TV Series - مسلسل ينابيع النهار )
  • 1986: Ya Helwa ( Sweetie - يا حلوة )
  • 1987: Assef ( Sorry - آسف ) – ( Assef la yogad hal akhar TV Series - مسلسل آسف لا يوجد حل آخر )
  • 2004: Amr Diab Greatest Hits (1986–1995)
  • 2005: Amr Diab Greatest Hits (1996–2003)
  • 2005: Mateftekrish ( Don't Even Think - ماتفتكريش )
  • 2016: Ahla Ma Ghanna Amr Diab 2004–2015 ( The best of Amr Diab 2004–2015 - أحلى ما غنى عمرو دياب

Marejeo

hariri
  1. "Bio". IMDb.
  2. 2.0 2.1 Frishkopf, Michael (2003). "Some Meanings of the Spanish Tinge in Contemporary Egyptian Music". Katika Plastino, Goffredo (mhr.). Mediterranean mosaic: popular music and global sounds (PDF). Routledge. ku. 145–148. ISBN 978-0-415-93656-9. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 27 Machi 2009. Iliwekwa mnamo 4 Juni 2009. {{cite book}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. eCelebrityFacts. "Amr Diab Biography", eCelebrityFacts.com. (en-US) 

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: