Anastasi II wa Antiokia

Anastasi II wa Antiokia (alifariki Antiokia, leo nchini Uturuki, 609) alikuwa askofu mkuu wa Antiokia kuanzia mwaka 599 hadi kifodini chake kinachosemekana kilichotokea kwa mikono ya Wayahudi waliokataa kulazimishwa na kaisari Fokas kuingia Ukristo[1][2][3].

Kabla ya hapo aliwasiliana mapema na Papa Gregori I kukiri imani sahihi akahimizwa naye kupambana na usimoni.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa kwenye 20 Aprili.[4]

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.