Angatando (pia angastrato; Kiingereza: stratosphere) ni tabaka mojawapo la angahewa ya Dunia[1]. Inaanza takriban kilomita 8 juu ya uso wa ardhi kwenye eneo la ncha za Dunia lakini juu ya ikweta inaanza kwa kimo cha kilomita 18; inaendelea hadi kimo cha kilomita 50 juu ya uso wa ardhi[2].

Matabaka ya angahewa

Katika angastrato, kiunyume na angatropo, halijoto inapanda juu pamoja na kimo. Hii inasababishwa na tabaka la ozoni iliyoko ndani yake. Ozoni hufyonza mnururisho wa urujuanimno kutoka nuru ya Jua na kuibadilisha kuwa joto[3].

Hii ni tofauti na angavurugu iliyoko chini yake. Huko halijoto inapungua kadiri ya kuongezeka kwa kimo. Pia katika angakati iliyoko juu ya tabakastrato halijoto inapungua kadiri ya kufikia juu zaidi.

Hakuna upepo wala mawingu katika angastrato, hivyo eropleni kubwa husafiri pale inapoanza kwenye kimo cha km 12 kwa safari za mbali ambako vurugu kutokana na upepo wa angavurugu zimeshapungua [4].

Marejeo

hariri
  1. [https://www.merriam-webster.com/dictionary/stratosphere Stratosphere], Merriam Webster dictionary
  2. "The Stratosphere - overview". scied.ucar.edu (kwa Kiingereza). University Corporation for Atmospheric Research. Iliwekwa mnamo 25 Julai 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "The Stratosphere - overview". scied.ucar.edu (kwa Kiingereza). University Corporation for Atmospheric Research. Iliwekwa mnamo 25 Julai 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Altitude of a Commercial Jet". Hypertextbook.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-31. Iliwekwa mnamo 2011-11-08.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angatando kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.