Matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara ni kundi la matatizo yenye sifa ya hisia muhimu ya wasiwasi na hofu.[1] Wasiwasi ni mahangaiko kuhusu matukio ya siku zijazo, na hofu ni athari kwa matukio ya sasa.[1] Hisia hizo zinaweza kusababisha dalili mwilini, kama vile mapigo ya haraka ya moyo, tetemeko[1], utovu wa usingizi, uchovu mwilini, hasira[2] n.k.

Sura ya mtu mwenye matatizo hayo kwa namna ya kudumu.

Kuna aina ya matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara kama vile tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara, hofu isiyo ya kawaida, tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara la utengano, hofu isiyo ya kawaida kwa sababu ya umati wa watu, tatizo la kiakili linalosababisha hofu kubwa ya ghafla, na kuchagua kutozungumza.[1] Tatizo hili hutofautiana kwa yanayotokea kwenye dalili zake.[1] Mara nyingi watu huwa na zaidi ya tatizo moja la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara [1].

Chanzo hariri

Chanzo cha matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara ni mchanganyiko wa vipengele vya jenetikia na mazingira.[3] Vipengele vya hatari ni pamoja na historia ya unyanyasaji wa mtoto, historia ya familia yenye matatizo ya kiakili, na umaskini.[4]

Matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara hutokea na matatizo mengine ya kiakili, hasa matatizo ya kiakili yanayosababisha huzuni kali kwa muda mrefu, tatizo la kiakili linalosababisha mfumo imara na mbaya wa kitabia na kufikiria na tatizo la kiakili linalosababisha matumizi mabaya ya dawa ili kuathiri hisia za mtu.[4] Ili kutambuliwa, dalili kwa kawaida zinahitaji kuonekana kwa angalau miezi 6, kuwa zaidi ya kinachoweza kutarajiwa kwa hali hiyo, na kupunguza utendakazi.[1][4]

Shida nyingine ambazo zinaweza kuwa na dalili sawa ni kama vile hali ya kuipa tezi shughuli nyingi kisha kusababisha mapigo ya moyo; ugonjwa wa moyo; matumizi ya kafeini, pombe, au bangi; na kujiondoa kwa dawa fulani, miongoni mwa nyingine.[4][5]

Tiba hariri

Bila matibabu, matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara husalia.[1][3] Matibabu yanaweza kuwa mabadiliko ya mfumo wa maisha, ushauri na dawa.[4] Ushauri kawaida huwa na aina ya tiba ya utambuzi kitabia.[4] Dawa kama vile dawa za kutibu huzuni, dawa ya kutibu wasiwasi na hofu (benzodiazepini) au dawa za kudhibiti mapigo ya moyo, zinaweza kuboresha dalili.[3]

Uenezi hariri

Karibu 12% ya watu wameathiriwa na tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara kwa mwaka fulani, na kati ya 5% na 30% wameathiriwa kwa wakati fulani maishani mwao.[4][6] Hutokea karibu mara mbili zaidi kwa wanaume na kwa kawaida huanza kabla ya umri wa miaka 25.[1][4] Za kawaida zaidi ni hofu maalum isiyo ya kawaida ambayo huathiri karibu 12% na tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara la kijamii ambalo huathiri 10% kwa wakati fulani maishani mwao.[4] Huathiri sana walio na umri wa kati ya miaka 15 na 35 na huwa nadra baada ya umri wa miaka 55.[4] Viwango huonekana kuwa vya juu Marekani na Ulaya.[4]

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 Diagnostic and Statistical Manual of Mental DisordersAmerican Psychiatric Associati. (5th ed.). Arlington: American Psychiatric Publishing. 2013. pp. 189–195. ISBN 978-0890425558. 
  2. Online Therapy (2018-09-10). Symptoms and Solutions for Stress, Anxiety and Anger Management (en-US). Online Therapy Reviews. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-08-15. Iliwekwa mnamo 2019-02-25.
  3. 3.0 3.1 3.2 Anxiety Disorders (March 2016). Jalada kutoka ya awali juu ya 27 July 2016. Iliwekwa mnamo 14 August 2016.
  4. 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 Craske, MG; Stein, MB (24 June 2016). "Anxiety.". Lancet. PMID 27349358. doi:10.1016/S0140-6736(16)30381-6. 
  5. "Psychiatric emergencies (part III): psychiatric symptoms resulting from organic diseases". Eur Rev Med Pharmacol Sci (Review). 17 Suppl 1: 86–99. 2013. PMID 23436670. Archived from the original on 10 March 2016.  Unknown parameter |vauthors= ignored (help); Unknown parameter |df= ignored (help)Kigezo:Open access
  6. Kessler (2007). "Lifetime prevalence and age-of-onset distributions of mental disorders in the World Health Organization–s World Mental Health Survey Initiative". World Psychiatry 6 (3): 168–76. PMC 2174588. PMID 18188442. 

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anxiety Disorder kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.