Apia ni mji mkuu wa nchi ya visiwani ya Samoa katika Pasifiki wenye wakazi 45,000. Mji uko kwenye pwani ya kaskazini ya kisiwa cha Upolu.

Kitovu cha Apia
Ramani ya Apia
Apia mnamo 1839
Bandari ya Apia mwaka 2003.

Apia ni bandari kuu ya Samoa, pia kitovu cha biashara na uchumi wake. Katika muda wa miaka 10 iliyopita biashara ilistawi vema mji ukakua. Kwenye mtaa wa Vaitele kuna viwanda vya vipuli vya magari, nguo na vinywaji.

Mtaa wa Mulinu'u ni eneo la mji mkuu wa kale uliopo sasa upande wa magharibi wa mji wa kisasa penye jengo la bunge.

Mji umekua kando ya mdomo wa mto Vaisigano penye kinga nzuri kwa meli.

Kusini kwa mji umepanda mlima Vaea (kimo cha mita 472).