Nguo ni kitambaa ambacho kinaweza kutumika kufunikia meza, kitanda n.k. lakini hasa kutengenezea mavazi mbalimbali yanayovaliwa na mtu kwa ajili ya kujisitiri, kwa sababu ya kutunza heshima yake na kujikinga dhidi ya baridi, jua, mvua n.k. Ndiyo sababu mara nyingi neno "nguo" linamaanisha mavazi yenyewe.

Kitambaa kilivyoshonwa.
Vitambaa vya Alpaca katika soko laOtavalo, Ecuador.
Duka la nguo huko Mukalla, Yemen.

Nguo huvaliwa kulingana na hali ya hewa na mazingira fulani, lakini pia kulingana na mitindo inayobadilikabadilika kadiri ya nyakati.

Historia ya nguo hariri

Kulingana na wanaakiolojia na wanaanthropolojia, nguo za kwanza zilikuwa manyoya, ngozi za wanyama, majani na nyasi. Uvaaji wa nguo hizi uliwasaidia binadamu haswa katika kujikinga na hewa baya, kujikinga na vumbi pamoja na dhoruba kali.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nguo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.