Axis Powers Hetalia
Axis Power Hetalia ni katuni ya Kijapani. Himaruya awali aliumba Hetalia kama "webcomic" na sasa tankōbon viwili vimechapishwa na kampuni liitwalo Gentosha Comics, cha kwanza lilitozwa tarehe 28 Machi 2008 na cha pili tarehe 10 Desemba 2008. Baadaye diski za maigizo("drama CDS") zilirekodiwa, na anime iliyoendelezwa na Studio Deen pia ilianza kusambazwa kwa mtandao.
Matukio ya kihistoria kuu yanayohusishwa katika tunzo hili yalitokea kati ya Vita Kuu I na Vita Kuu II Mara nyingi kuna matumizi ya kejeli, kinaya, tamthilia na kichekesho kushughulikia matukio ya kihistoria yanayojulikana na yasiyojulikana mno. Mahusiano ya kihistoria, kisiasa na kijeshi kati ya nchi yaliwasilishwa katika Hetalia kwa kutumia maingiliano ya kipenzi na maingiano kati ya wahusika; toleo la "webcomic" hasa hurejelea maingiliano ya kijeshi na kiuchumi kwa kutumia fumbo.
Wahusika Wakuu
haririHadi sasa, zaidi ya nchi 40 zimewasilishwa kama wahusika binadamu. [1] Katika Hetalia, wahusika hawa kwa kawaida wanajulikana kwa jina la nchi wanayowasilisha.
Ujerumani na Wenzake ("Axis Powers")
hariri"Axis Powers" ni kundi la wahusika linalozingatia nchi za Ujerumani, Italia, na Ujapani, ambao pia ni wahusika wakuu wa hadithi. Nchi nyingine kama Austria ambazo zilisimama na Ujerumani katika vita yanawasilishwa katika hadithi pia.
- Kaskazini Italia (イタリア- Italia)
- Italia, mhusika mkuu, ni kijana wa furaha na asiyepata wasiwasi kwa urahisi. Kulingana na sehemu ya hadithi inayozingatiwa, anawasilishwa kama mtoto mchanga mjukuu wa Himaya la Roma (rejelea Roma ya Kale), anayetambuliwa kama mhusika hodari kuliko wengine, na kama askari mwoga na terema ambaye mara nyingi hutegemea Ujerumani kutatua masuala. Ustadi wake katika sanaa na upendo wake wa pasta na pizza ni marejeo kwa utamaduni wake wa Kiitaliano. Italia anawakilisha nusu ya nchi ya Italia iliyomo upande ya kaskazini, na kaka yake anawakilisha nusu iliyomo kusini. Majina yao kamili ni Italy Veneziano na Italia Romano. Daisuke Namikawa ndiye anayeigiza sauti la Italia katika anime.
- Ujerumani (ドイツ- Doitsu)
- Ujerumani ni mfanyikazi anayejitahidi katika kazi, mfanisi, mkiritimba, na asiyemcheshi. Ujerumani ni mhusika anayeheshimiwa sana(Primus inter Pares) miongoni mwa nchi za Axis Powers, na anachukua jukumu la mafunzo ya Italia na Ujapani. Tabia jingine Ujerumani analo ni uzuzu katika mwingiliano na watu wengine na kwa ajili hii huogopa sana kwamba asipotenda mambo kwa njia fulani ataangamia. Ingawa ya hayo, yeye anapata amekuza urafiki na Italia, ambaye anaelezea kama rafiki yake wa pekee. Kuna kivutio cha kipenzi kati ya Ujerumani na Italia ya Kaskazini inayogusiwa katika hadithi, kama vile Ujerumani kuhisi moyo wake ukidunda kwa kasi wakati ambako Italia anajadili naye kuhusu jambo la kibinafsi, lakini kivutio hiki hakijathibitisha moja kwa moja. Saa moja anabainisha kwamba ana mkubwa mwendawazimu ("crazy boss"), akirejelea kiongozi wa Ujerumani Hitler. Hiroki Yasumoto ndiye anayeigiza sauti la Ujerumani katika anime.
- Ujapani (日本)-Nihon)
- Ujapani ni mhusika anayejitahidi katika kazi na ni mtenga. Huonyeshwa kuwa zuzu katika tamaduni za nchi za magharibi ("Western World") , na wakati mwingine hupata mshtuko kutokana na mwonjo wa tamaduni hizo. Yeye huwasilishwa kama kijana aliye na nywele eusi na macho hudhurungi, sifa ya kawaida ya kimwili kati watu wa asili ya Kijapani. Ujumla, yeye ni mtulivu na mwenye tabia za mfanyibiashara mzee. Hiroki Takahashi ndiye anayeigiza sauti la Ujapani katika anime.
Mataifa ya ushirikiano ("Allied Forces")
haririKundi hili lilizingatia nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uchina na Urusi. Katika mikutano yao ya vita wahusika hawa huonyeshwa kama wasioweza kupata maafikiano. Nchi zingine kama Kanada ambazo zilisimama na Mataifa ya Ushirikiano katika vita zinawasilishwa katika hadithi pia.
- Marekani (アメリカ- Amerika)
- Marekani ni mhusika mchangamfu na mkaidi. Katika hadithi, alilelewa na Uingereza na baadaye kuipigia uhuru wake. Alijitangaza kama kiongozi wa kundi lake, tamko lake la kawaida ("catchphrase") ni, "Mimi ni Shujaa!" ('I am the hero!'). Mawazo yake kwa ajili ya kutatua matatizo ya kimataifa mara nyingi ni ya ajabu, lakini kawaida hayatii maoni ya wengine. Mawazo ya Marekani huwa ya kushangaza, lakini ni mara chache ambapo mawazo haya yanafua dafu. Ana hofu mwingi ya vizuka lakini hofu hii inapingana na urafiki yake na kijivu jinale Tony, ambaye anaishi katika nyumba yake. Marekani mara nyingi huonekana akishika aina ya chakula kiitwacho "hamburger" (nyama iliotiliwa kati ya mkate), au akila wakati anazungumza. Katsuyuki Konishi, ndiye anayeigiza sauti la Marekani katika anime.
- Uingereza (イギリス- Igirisu)
- Hurejelewa kama aina ya mhusika anayejulikana kama tsundere, hawa ni wahusika ambao huonekana kama watu wagomvi na wanaokasirika kwa urahisi lakini pia wanaweza kuwa wakarimu na wachangmfu kutegemea na wahusika ambao wana mwingiliano nao. Katika hadithi, anawasilishwa kama kijana anayekasirika kwa haraka. Alikuwa mharamia awali, lakini sasa ni muungwana asiyewaamini watu wengine na ni mteuzi. Baadhi ya sifa zake mashuhuri ni kuwa mpishi mbaya, kutumia matusi, na uwezo wa kuona viumbe kimungu. Uingereza ameonyeshwa pia kuwa mchawi anayefanya laana kwa maadui wake. Uingereza ni adui wa Ufaransa -ambaye amekuwa na ghiliba naye kutoka zamani- na Amerika ambaye alimlea zamani. Sifa zake kimwili ni kuwa mfupi na nyusi nene
- Ijapokuwa jina lake linamaana "Britain" ni kawaida kutafsiriwa kama "Uingereza" kwa watafsiri mashabiki na Hidekaz mwenyewe, mhusika Uingereza hutambuliwa kwa bendera ya Uingereza, kwa sababu katika lugha ya kigeni "Uingereza" ni kisawe cha "Great Britain" na "UK" Katika toleo moja la hadithi anabainisha kwamba yeye ana kaka aitwaye Scotland [2] na katika toleo lingine,Uingereza anataja ndugu zake wakubwa (huenda ni Scotland na Wales na Jamhuri ya Ireland). Noriaki Sugiyama ndiye anayeigiza sauti la Uingereza katika anime.
- Ufaransa (フランス- Furansu)
- Ufaransa ni mhusika mchangamfu na mpenzi. Katika hadithi tunaona kuwa yeye na Uingereza wamekuwa na ghiliba kwa miaka mingi. Hata hivyo, kufuatilia sifa yake ya uzinifu yeye hupenda kutoa dokezo yanayozingtia ngono kwa nchi kadhaa, ikiwemo Uingereza. Ufaransa anaelezea historia yake ndefu ya kutoshinda katika vita kwa kusema kuwa anadhihakiwa na Mungu. Anajihesabia kama ndugu mkubwa miongoni mwa mataifa ya Ulaya na ni anajulikana kwa cheti hiki kwa baadhi yao, ingawayeye hurejealea Uhispania kama ndugu wake mkubwa. Mara nyingi huwasilishwa akibeba waridi, aidha akilishika mkononi mwake au akilitumia kufunika sehemu zake za siri wakati anatembea uchi. Masaya Onosaka ndiye anayeigiza sauti la Ufaransa katika anime.
- Uchina (中国- Chūgoku)
- China ni moja ya mataifa kongwe, asiyekufa na mwenye umri wa miaka elfu kadhaa, huonekana kama ni ndugu mkubwa miongoni mwa mataifa ya Asia ya Mashariki. Kwa sababu ya Sino-Soviet Split yeye hamuamini Urusi. Uchina hupenda vyakula vya aina mbalimbali, kwa ajili hii ana upendo wa ladha fulani na hukasirika kama vyakula vina ladha inayofanana. Ni shabiki wa Hello Kitty(mhusika aliyezalishwa na kampuni liitalo Sanrio) na humalizia kila sentensi na kiishio-aru, lakini anapoongea na Uingereza hubadili kiishio na kutumia -ahen, ambayo inamaanisha afyuni kwa njia hii anazingatia Vita ya Afyuni. Yeye pia ana muda kovu ndefu mgongoni mwake kutokana na Ujapani kumathiri wakati wa Vita baina ya Uchina na Ujapani I mara nyingi anawasilishwa na aina ya dubu inayopatikana katika nchi za Asia ya Mashariki (pandas). Yuki Kaida ndiye anayeigiza sauti la Uchina katika anime.
- Urusi (ロシア- Roshia)
- Hurejelewa kama aina ya mhusika anayejulikana kama yandere. Huyu ni mhusika ambaye awali anawasilishwa kuwa na ukarimu na upole lakini baadaye hubalika na kuwa katili wa ajabu. Yeye ni mrefu miongoni mwa mataifa yote, lakini ana hatia na ukatili ya mtoto. Anapenda aina ya pombe jinalo vodka na ua la aina la alizeti. Humchukia General Winter kwa sababu licha ya kutumia baridi kumfaidisha katika vita, yeye hushambuliwa kila mwaka naye katika msimu wa baridi. Urusi ana uso wenye ukarimu, lakini alirukwa na akili kwa ajili ya kakamizi kutokana na umwagaji mwingi wa damu katika historia yake. Mataifa mengine yanamwoqogopa, hasa kundi la nchi tatu jinalo "Baltic Trio" (Lativia, Litwania, na Estonia), ambao anapenda kuwanyanyasa kimwili na kihisia. Saa zingine hupenda kuwafuata nchi zingine, hasa Uchina, akivalia kama dubu ya aina ya panda. Urusi pia ana dada wawili: dada mkubwa , Ukraine na dada mdogo, Belarus. Huwa mlegevu na husononeka anapowaza juu ya Ukraina ambaye ana matiti makubwa mno(jambo hili linambabaisha) na Belarus ambaye ni mnyanyasaji anayependa kurejelea matarajio ya kumlazimisha Urusi amuoe. Inaonekana kuwa Belarus ni nchi kamwe ambayo Urusi anahofia. Urusi hupa ahadi ya kwamba hatimaye "Wote watakuwa moja pamoja na Urusi". Msemo mwingine wake ni, "kolkolkolkol", ambao hutumika anapokasirika. Urusi ni mara nyingi huonekana akibeba buruma la chuma. Yasuhiro Takato ndiye anayeigiza sauti la Uchina katika anime.
Vyombo vya habari
haririManga
haririKibonzo cha mtandao ya asili ya Hetalia: Axis Powers ilichukuliwa katika tankōbon mbili na kuchapishwa na Gentosha Comics. Toleo la kwanza lilitolewa tarehe 28 Machi 2008 na la pili tarehe 10 Desemba 2008. Tankōbon la pili lilitolewa kama toleo la kawaida na toleo maalum ambalo lilikuwa pamoja na kijitabu cha ziada. [3]
Diski za Uigizaji ("Drama CDs")
haririHadi sasa, diski nne zimetolewa. Ya kwanza ilitolewa tarehe 15 Agosti 2008, ya pili, 24 Oktoba 2008, ya tatu on 29 Desemba 2008, na ya nne tarehe 3 Juni 2009. [4]
Anime
haririAnime ya Hetalia: Axis Powers yenye vipindi 26 ilitangazwa tarehe 24 Julai 2008. [5] Iliyoongozwa na Bob Shirohata (aliyeongoza Gravitation, Diamond Daydreams) na ni iliendelezwa na Studio Deen. Awali ilikuwa imepangwa kutangazwa kwa stesheni jinalo Kids Station tarehe 24 Januari 2009 lakini baadaye ilibatilishwa. Ubatilishi uliathiri tangazo katika Kids Station lakini tangazo katika rununu na mtandao uliendelea. Kigambo kilitokana na waandamanaji waliodhani kuwa mhusika aliyewasilisha Korea aliaibisha wananchiwa Korea na nchi yote kwa ujumla. Kids Station walidai kwamba sababu la ubatilishi haukutokana na waandamanaji lakini hawakutoa maelezo mengine. Msimu wa vipindi ya pili ya Hetalia: axel Powers ilitangazwa tarehe 16 Aprili 2009, na msimu ya tatu ilitangazwa tarehe 10 Desemba 2009. [6] [7] [8]
Filamu
haririFilamu kuhusu wahusika wa hadithi ilitangazwa tarehe 23 Septemba 2009. [9] Itatolewa mwaka 2010.
Utata juu ya yaliyomo
haririKihistoria, Japan ilivamia na kuiba vitu Korea, hivyo kusababisha migogoro mikubwa kati ya nchi hizo. Hata hivyo, katika katuni hii, mtunzi anaeleza kwamba Korea ya Kusini anapenda bendera ya Japan, ifuatavyo wengine, na anasisitiza chochote ni chao. Pia, mwandishi alieleza Korea kama kuipotosha au mtu mambo ambao mapigo Japan. Lakini hii si kweli wakati wote. Kuna mengi ya unyenyekevu katika Korea kuliko nchi nyingine yoyote. Hivyo kulikuwa na utata mkubwa katika Korea.
Angalia Pia
hariri- Afghanis-tan - a manga yenye Nguzo sawa na APH, lakini inalenga Afghanistan na nchi jirani.
Marejeo
hariri- ↑ "Character listing" (kwa Japanese). Hidekaz Himaruya. Iliwekwa mnamo 30 Januari 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ 新大陸アメリカ争奪合戦 (Japanese). Hidekaz Himaruya. Retrieved on 17 Aprili 2009.
- ↑ "Gentosha's official Hetalia: Axis Powers manga site" (kwa Japanese). Gentosha. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-15. Iliwekwa mnamo 1 Januari 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Official site for the Hetalia Axis Powers anime" (kwa Japanese). Iliwekwa mnamo 18 Juni 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Hetalia Axis Powers Web Manga Gets TV Anime". Anime News Network. 24 Julai 2008. Iliwekwa mnamo 1 Januari 2009.
- ↑ "Hetalia Anime's Second Season Green-Lit (Updated)". Anime News Network. 2009-04-15. Iliwekwa mnamo 2009-04-16.
- ↑ "Hetalia Anime's Third Season Green-Lit (Updated)". Anime News Network. 2009-12-10. Iliwekwa mnamo 2009-12-10.
- ↑ "Hetalia Hetalia Axis Powers 3rd Season Confirmed". The Banzai! Effect. 2009-12-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-16. Iliwekwa mnamo 2009-12-10.
- ↑ "Hetalia Axis Powers Film Green-Lit for 2010". Anime News Network. 23 Septemba 2009. Iliwekwa mnamo 23 Septemba 2009.
Viungo vya nje
hariri- Manga's official website "Kitayume" (Kijapani)
- Hetalia: Axis Powers Ilihifadhiwa 21 Aprili 2012 kwenye Wayback Machine. kwa Gentosha Comics (Kijapani)
- Anime's official website (Kijapani)
- Axis Powers Hetalia (manga) at Anime News Network's Encyclopedia