Ayman Mohyeldin (amezaliwa 1 Mei 1979) ni mwanahabari Mwarabu wa Marekani ambaye yuko mjini Arabuni anayefanyia kazi Al-Jazeera.[1] anayeripotia kutoka Gaza. Hapo awali alikuwa akisimamia kutengeneza vipindi alipokuwa akifanya kazi CNN na NBC. Ayman alikuwa mmoja wa waandishi wa habari wa kwanza kutoka magharibi kuruhusiwa kuingia Iraq na Serikali ya awali ya Iraq ili kuripoti kuhusu kesi ya Rais wa Iraq Saddam Hussein iliyohusu uhalifu dhidi ya ubinadamu.[1] Hivi karibuni, Ayman aliwahi kuripoti kuhusu vita kati ya Israel na Gaza mnamo Desemba 2008.[2] Yeye alikuwa mwandishi wa kwanza kutoa taarifa kwenye mtandao kuhusu vichuguu ambavyo vilitumiwa kimagendo kupitisha silaha na watu mpakani Misri na Gaza. Mpaka wa leo, njia hii ni muhimu inayotumika kuingiza dawa, chakula na mafuta[3] mjini Gaza

Ayman Mohyeldin

Amezaliwa 18 Aprili 1979
Cairo, Misri
Nchi Marekani
Kazi yake Mwanahabari
Mwajiri NBC

Wasifu hariri

Ayman alizaliwa mjini Cairo, Misri. Babake ana asili ya kutoka Misri na mamake ni wa Palestina. Yeye alikulia nchini Misri na Marekani lakini ameishi sana katika nchi za Kiarabu na amewahi kuishi miaka miwili nchini Iraq (2003-2005) kama mwanahabari wa kigeni alipokuwa akifanya kazi CNN.[4] Hivi sasa, anaishi jijini Gaza na ni mwanahabari mkuu wa Al-Jazeera ya Kiingereza.[1] Ayman hakusomea rasmi masomo ya uandishi habari, bali alisomea Siasa (International Politics) katika chuo kikuu cha American University mjini Washington DC. Alipata shahada yake ya kwanza ya Uhusiano wa Kimataifa kwa lengo la Umoja wa nchi za Ulaya na shahada yake ya pili kuhusu Siasa kwa lengo na azimio la amani na migogoro. Ripoti yake ya utafiti alipokuwa chuo kikuu "The News Media Paradigm in the Wars on Terrorism" ilitambulika na kukubaliwa na International Association of Media Researcher's Conference mjini Barcelona, Hispania (2002)

Maisha ya awali hariri

Ayman alianza kufanya kazi kwa NBC News. Baada ya kuacha kusomea Sheria, Ayman alianza kazi kama msaidizi jijini Washington DC. Yeye anadai kuwa kufanya kwake kama msaidizi kulileta athari kubwa kwa maisha yake kama mwandishi wa habari. Kazi yake ya kwanza halisi ilianza muda mfupi baada ya mlipuko wa 9 / 11.[4] Katika mahojiano na PRWeek, Ayman anaeleza vile maisha yake ya hapo awali yalivyoathiri kazi yake ya sasa ya kuwa mwanahabari: "Kwa bahati mbaya, Septemba 11 ilitokea, na hapakuwa na watu wengi waliojua lugha na waliokuwa na ujuzi uliotakikana katika nchi za Kiarabu. Nilipata uzoefu mwingi kwa sababu ya ujuzi wa lugha yangu. Nilipewa mchanganyiko wa kazi nifanye ambayo msaidizi wa kawaida asingepata fursa kama hii. Nilianza kufanya uchunguzi mkubwa wa 9 / 11 na kila aina ugaidi uliohusiana nao ... Mara nyingi, nilikuwa nikifanya kazi ya kutafsiri, lakini pia niliwahi kutunga mandhari au hadithi zilizohusika na nchi za Kiarabu au zilitaka ujuzi wa lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo nilipata uzoefu mkubwa usioaminika nilipokuwa na umri mdogo.[4]

Kazi ya hivi karibuni hariri

Ayman amewahi kutoa habari za matukio makubwa katika nchi za Kiarabu kama vita vya Iraq, Uchaguzi wa kwanza uliohusisha wapigianaji urais walikuwa wengi nchini Misri 2005, Israeli kutoka Gaza na uchaguzi wa Palestina mwaka wa 2005 katika Ukanda wa Gaza. Amesafiri sana katika nchi za Kiarabu akiripotia kuhusu bomu la Sharm al-Sheikh (Julai 2005) na kuripuliwa kwa Hoteli ya Jordan (Novemba 2005).

Kama mtayarishaji wa habari, Ayman alikuwa mwandishi wa kwanza kuingia kwenye stesheni za nyuklia nchini Libya baada kutoa "Col". Muammar al-Gaddafi alitangaza kwa mahojiano kuwa Libya imeachana na mipango ya WMD.[4] Ripoti yake aliotoa alipokuwa CNN "Iraq:Progress reeport" iliyohusu mapambano ya kila siku wakati wa vita vya Iraq ilichaguliwa (lakini haikushinda) tuzo la Emmy. Alihudumu kama mtayarishaji msaidizi kwa NBC News Special ambayo pia ilipokea (lakini haikushinda) tuzo la Emmy iliyohusu "Ship at War: Inside the Carrier Steennis" & "Inside the Real West Wing." [4] Yeye pia anajulikana kwa kuripoti kuhusu Hija ya kila mwaka ya Kiislamu (Hajj) inayofanyika Makka na alikuwa akishiriki katika CNN Specials "Islam: The Struggle Within" na "Hajj: A Spiritual Journey."

Hivi sasa, yuko Gaza akiripotia kuhusu janga lililoko huko.

Marejeo hariri

[1][2][3][4][5][6][7][8][9][10][11][12]

Viungo vya nje hariri

 1. Gazze'yi tek başına savunan gazeteci! Archived 19 Februari 2012 at the Wayback Machine. Haber vaktim
 2. Gaza Strip: In praise of Al Jazeera, Part 1 LA Times
 3. Gaza Strip: In praise of Al Jazeera, Part 2 LA Times
 4. Kwa civilians, 'There is No Safe Zone Gaza' NPR
 5. Gideoni Levy / My hero of the Gaza war Haarretz
 6. Twilight Zone / Trumpeting for war Haarretz
 7. War on Gaza: More Death Threats to Haaretz's Gideon Levy over Al Jazeera Article Archived 18 Julai 2009 at the Wayback Machine. BBCNews
 8. The war that made al Jazeera English 'different' Archived 26 Julai 2014 at the Wayback Machine. The National
 9. Al Jazeera provides an inside look at Gaza conflict The International Herald Tribune
 10. Al Jazeera English Beats Israeli's Ban on Reporters in Gaza with Exclusive Coverage The HUFFINGTON POST
 11. Al-Jazeera becomes the face of the frontline Financial Times
 12. Gazze büyük bir hapishane Archived 19 Februari 2012 at the Wayback Machine. Haber vaktim