B
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
B ni herufi ya pili katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Beta ya Kigiriki.
Maana za alama B
haririHistoria ya herufi B
haririKisemiti asilia picha ya ramani ya nyumba |
Bet ya Kifinisia |
Beta ya Kigiriki | B ya Kilatini |
---|---|---|---|
Kama herufi nyingine za alfabeti ya Kigiriki beta imetoka katika alfabeti ya Wafinisia iliyokuwa alfabeti ya kwanza ya dunia. Wafinisia waliendeleza mwandiko wa kikabari wa kale uliokuwa mwandiko wa silabi na kuifanya alfabeti ya herufi moja-moja.
Faida ya alfabeti ni ya kwamba inahitaji alama chache kulingana na mwandiko wa silabi mwenye alama kwa kila silabi ya lugha fulani au mwandiko picha unaohitaji maelfu ya alama za picha.
Bet ya Wafinisia
haririWafinisia walichukua alama ya ramani ya nyumba wakairahisisha na kuiita kwa neno lao "bet" lenye maana ya "nyumba" lakini walisoma tu "b" yaani sauti ya kwanza katika neno hili. Hivyo walifanya picha ya nyumba kuwa herufi iliyo alama ya sauti "b". Herufi ilitazama upande wa kushoto pa kwa sababu mwendo wa kuandika ulikuwa kuanza upande wa kulia klwenmda kushoto jinsi ilivyo katika lugha za Kisemiti za Kiebrania na Kiarabu.
Kufuatana na kalamu tofauti (kama ni kuandika kwa kijiti kwenye udongo wa ufinyanzi au kwa wino kwenye karatasi) umbo la herufi likaandikwa kwa michirizo au zaidi kwa kona.
Beta ya Wagiriki
haririWagiriki walipokea alfabeti kutoka Wafinisia na pia jina la herufi hii. Wakabadilisha kidogo jina kuwa "beta" badala ya "bet". Lakini katika lugha yao hawakuelewa tena maana asilia iliyokuwa "nyumba". Kwao ilikuwa alama ya sauti tu.
Mwanzoni waliandika herufi kwa kutazama upande wa kushoto kama walivyofanya Wafinisia lakini katika karne za baadaye herufi iligeuzwa na kuandikwa mwishowe jinsi tunavyozoea leo.
B ya Kilatini cha Waroma wa Kale
haririWaroma wa Kale walipokea alfabeti kutoka Wagiriki na kuibadilisha kwa mahitaji yao. Beta ikaitwa nao kwa sauti yake tu yaani "b" badala ya neno "beta".