Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz


L ni herufi ya 12 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Lambda ya alfabeti ya Kigiriki.

Maana za L

hariri

Historia ya L

hariri
Kisemiti asilia
Fimbo la kuchungia ng'ombe
Kifinisia
Lamed
Kigiriki
Lambda
Kietruski
L
Kilatini
L
         

Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha fimbo la kuchungia ng'ombe. Wafinisia walirahisihsa alama hiyo na kuiita kwa neno lao la fimbo hili "lamed". Wakaitumia kama alama ya sauti "l". Wagiriki wa Kale wakaipokea kama "Lambda" na kubadilisha umbo lake kuwa kama paa ya nyumba.

Waetruski walipendelea umbo la kifinisia kwa kuiandika kama alama ya sauti "l". Waroma wa Kale wakageuza alama na kunyosha mikono yake kuwa L jinsi iliovyo hadi leo.

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu L kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.