Beta (Kigiriki: Βήτα, Β/β) ni herufi ya pili katika alfabeti ya Kigiriki. Ilikuwa pia na maana ya alama kwa namba 2. Inaandikwa Β (herufi kubwa ya mwanzo) au β (herufi ndogo ya kawaida).

Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Katika Kigiriki cha kale ilitaja sauti ya "B". Katika Kigiriki cha kisasa imekuwa alama ya sauti "V".

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fizikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya pili katika pembetatu.

Katika falaki inatumiwa sana kwa hesabu ya nyota katika kundinyota. Katika mfumo wa Bayer inataja nyota angavu ya pili katika kundinyota fulani. Kwa mfano nyota yetu jirani katika ulimwengu inaitwa "Alfa Centauri". Imeitwa hivyo kwa sababu inang'aa kushinda nyota zota za kundinyota la Centaurus. Inayofuata ni "Beta Centauri" na kadhalika. Hivyo Rasi Madusa (en:Algol) ilipokwa jina la Bayer "Beta β Persei" kwa sababu ni nyota angavu ya pili katika kundinyota laFarisi (Perseus).

Katika programu za kompyuta "toleo la beta" (=beta-version) humaanisha toleo la awali la programu. Wahariri wanaitoa kama imeshakamilika lakini kabla ya kuiuza wanatoa nakala kwa majaribio ili makosa yaonekana.