Baraza la Muziki la Taifa (kifupi: BAMUTA), lilianzishwa na serikali ya Tanzania mwaka 1974. Lengo lake lilikuwa ni kusimamia biashara ya muziki nchini, katika muktadha mpana zaidi uliyokusudia kutengeneza utambulisho imara wa Taifa.[1] Kwa upande mwingine, ilikuwa kipengele muhimu cha Ujamaa, toleo la Rais Julius Nyerere la Ujamaa wa Afrika. Taasisi kama hizi zilianzishwa pia ili kuongoza katika Nyanja ya utamaduni wa taifa, ikijumusha uenezi wa lugha ya Kiswahili nchi nzima (kupitia kwa Baraza la Kiswahili la Taifa) na maendeleo ya sanaa ya kitanzania (Baraza la Sanaa Tanzania: BASATA). Wazo kuu lilikuwa kutengeneza utamaduni mpya kwa wafanyakazi na wakulima wa nchi huru kutoka kwa urithi wa ukoloni na utamaduni wa ubepari.

BAMUTA ilikuwa na jukumu la kuweka sera za muziki za taifa, zilizolenga kudhibiti uagizaji wa muziki na ilitoa leseni za disko na klabu. Pia ilitaka serikali iweke mipango madhubuti pamoja na kudhibiti muziki maarufu wa Tanzania. Kwa mfano, kuagiza muziki wa kigeni kwa ujumla ilipigwa marufuku isipokua muziki kutoka Zaire.

Chini ya vizuizi kama hivyo, na sababu ya serikali kukuza ubunifu wa muziki, bendi nyingi ziliundwa na mitindo mipya ya muziki wa kiafrika iliibuka, hasa ndani ya biashara ya muziki wa dansi (dance music).

Mwaka 1984, BAMUTA ilifutwa na kuunganishwa na BASATA.[2]

Marejeo hariri