Ujamaa ni siasa iliyoanzishwa kwa misingi ya sera za Julius Nyerere za maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi katika Tanzania punde tu baada ya Tanganyika kupata uhuru kutoka Uingereza mwaka 1961.

Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Mwaka 1967 Rais Nyerere alichapisha mwongozo wa maendeleo yake, ambao uliitwa Azimio la Arusha, ambapo alionyesha haja ya kuwa na mtindo wa Kiafrika wa maendeleo; huo ukawa msingi wa Usoshalisti wa Afrika.

Maana hariri

Ujamaa linatokana na neno la Kiswahili linalomaanisha familia au jamii na hujulikana kwa sifa kadhaa muhimu, yaani mtu anakuwa mtu kwa kupitia watu au jamii.

Nyerere alitumia Ujamaa kama msingi wa mradi wa maendeleo ya taifa. Aliitafsiri dhana ya Ujamaa kuwa mfumo wa usimamizi wa kisiasa na wa kiuchumi kwa namna mbalimbali:

  1. Kuweko kwa mfumo wa chama kimoja chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kusaidia katika kuimarisha mshikamano wa kujitegemea kwa Tanzania iliyokuwa tu imejipatia uhuru.
  2. Ustawishaji wa usawa kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kuweko kwa demokrasia kuu; kukomesha ubaguzi kwa misingi ya hali ya mtu; na kuzifanya sekta muhimu za uchumi kufikia taifa zima[1].
  3. Kupeleka uzalishaji katika vijiji, ambapo ilifanya uwezo wa uzalishaji wa aina zote kufanyika kwa pamoja.
  4. Kukuza kujitegemea kwa Tanzania kwa njia mbili: mabadiliko ya kiuchumi na mitazamo ya kiutamaduni. Kiuchumi, kila mtu angekifanyia kikundi chote kazi na kujifanyia yeye mwenyewe; kiutamaduni, ni lazima Watanzania wajifunze kujikomboa kutoka kwa utegemezi wa nchi za Ulaya. Kwake Nyerere, hii ilijumuisha Watanzania kujifunza kujifanyia mambo wao wenyewe na kujifunza kuridhika na kile ambacho wangeweza kufikia kama nchi huru.
  5. Utekelezaji wa elimu bila malipo na ya lazima kwa Watanzania wote ili kuwahamasisha wananchi kuhusu kanuni za Ujamaa[1].

Utekelezaji hariri

Uongozi wa Julius Nyerere uliivutia Tanzania macho na heshima ya kimataifa kutokana na msisitizo wake wa maadili kama msingi wa maamuzi ya siasa. Chini ya Nyerere Tanzania ilipiga hatua kubwa katika vipengele mbalimbali vya maendeleo: vifo vya watoto vilipungua kutoka 138 kwa 1000 waliozaliwa hai mwaka 1965 hadi 110 mwaka 1985; tarajio la kuishi lilipanda kutoka miaka 37 (1960) hadi 52 (1984); uandikishaji wa wanafunzi katika shule ya msingi ulipanda kutoka 25% (16% tu kwa watoto wa kike) mwaka 1960 hadi 72% (85% kwa watoto wa kike) mwaka 1985 (ingawa idadi ya wananchi ilikuwa inaongezeka kwa kasi); asilimia ya watu wazima waliojua kusoma na kuandika ilipanda kutoka 17% mwaka 1960 hadi 63% mwaka 1975 (juu sana kuliko nchi nyingine za Afrika) ikaendelea kupanda.[2]

Hata hivyo Ujamaa (kama vile mipango mingine ya uzalishaji wa pamoja) ulipunguza uzalishaji hata kutia shaka juu ya uwezo wake wa kustawisha uchumi.[3]

Hatimaye sababu mbalimbali zilifanya Ujamaa uonekane umeshindikana kiuchumi. Kati ya hizo, tatizo la kimataifa la mafuta miaka ya 1970, anguko la bei ya bidhaa zilizozalishwa nchini (hasa kahawa na katani), utovu wa uwekezaji kutoka nje ya nchi na vita vya Uganda-Tanzania miaka 1978-1979 vilivyofyonza sana mtaji muhimu, na miaka miwili mfululizo ya ukame.

Kufikia mwaka 1985 ilikuwa wazi kwamba Ujamaa ulishindwa kutoa Tanzania nje ya ufukara wake; Nyerere alitangaza kuwa atang'atuka asigombee tena urais katika uchaguzi wa mwaka huohuo.

Ujamaa ulivunjwa (ingawa si kinadharia) mwaka 1985 wakati Nyerere alipomwachia mamlaka Ali Hassan Mwinyi aliyeingiza nchi katika taratibu za soko huria[4].

Hoja dhidi yake hariri

Nyerere alitumia Sheria ya Kuzuia Kutiwa Nguvuni bila sababu kukandamiza vyama vya wafanyakazi na kuwakamata wapinzani kikatili kupindukia; walioathiriwa huhesabiwa kuwa maelfu.

Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International yalipiga kampeni dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania[5].

Vyombo vya habari nchini vilidhibitiwa kwa kunyimwa usajili rasmi.

Serikali iliwalazimishwa watu kuhamia mashamba ya pamoja, jambo ambalo lilitatiza shughuli za kilimo na uzalishaji.

Wengine walilazimishwa, kwa mfano, kwa kuchoma vijiji vyao. Nyumba ziliteketezwa kwa moto au kubomolewa, wakati mwingine pamoja na mali ambayo familia hizo zilikuwa nayo kabla ya Ujamaa[6].

Watu walipoteza heshima kwa utamaduni na maeneo kama vile makaburi ya mababu zao[6].

Polisi na wanajeshi waliojihami kwa silaha walitumika katika uhamisho wa watu[6]. Tanzania iligeuka kutoka taifa la wakulima waliojitahidi kukidhi mahitaji yao na kuwa taifa la wakulima walioangamia kwa njaa kwa pamoja.

Taifa lilinusurika kwa kutegemea msaada ya kigeni ya chakula ambacho walipewa tu watu waliokubali kujiunga na Ujamaa[6].

Serikali iliwapa ahadi ambazo baadaye ziligeuka kuwa uongo.

Uchumi ulianguka. Kiasi kikubwa cha utajiri wa nchi aina ya mijengo na kuboresha miundo ya ardhi (mashamba, miti ya matunda, nyua) iliharibiwa au kutelekezwa kwa lazima [6].

Mifugo waliibwa, kupotea, kupata magonjwa, au kufa[6].

Suleman Sumra aligundua kuwa mavuno katika mashamba ya Ujamaa kwa pamoja yalikuwa chini kwa asilimia 33-85 kuliko yale ya mashamba yaliyomilikiwa kibinafsi. Kwa wastani yalikuwa chini kwa asilimia 60. Wakulima wa pamoja hawakuwa na motisha za kufanya kazi[6].

Hali ya nchi ilienea haraka na kuathiri karibu kila sekta. Mwaka 1967, ustawishaji wa taifa ulibadilisha serikali na kuifanya mwajiri mkubwa zaidi katika nchi. Ilihusika katika kila kitu, kuanzia kufanya mauzo ya rejareja hadi biashara ya kuuza na kuagiza bidhaa kutoka ng'ambo na hata uokaji, na kuleta mazingira muafaka kwa ufisadi[7].

Ukiritimba na taratibu zisizoeleweka ziliongezeka na viwango vya juu vya kodi kuwekwa[7].

Fedha za umma zilitumika vibaya na kuweka kwa matumizi yasiyo na faida[7]. Uwezo wa kununua ulipungua kwa kiwango kikubwa mno na hata bidhaa muhimu zikawa hazipatikani[7].

Mfumo wa kutoa vibali uliwaruhu maafisa wakuu kuchukua rushwa kubwa ili kutoa vibali[7]. Msingi wa mfumo wa ufisadi ukawa umewekwa[7].

Barabara ziliharibika na kuwa kati ya barabara mbovu zaidi barani Afrika.

Sekta ya viwanda ikadidimia. Kampuni ya mgodi iliyomilikiwa na serikali ikaonekana kushindwa[8].

Benki ya Dunia pia imekosolewa kwa kuchangia mpango huo: "Nchini Tanzania, kwa mfano, Benki hii ilitoa fedha kwa kampeni ya udikteta wa Julius Nyerere unaoitwa Ujamaa, ni mfano wa mfumo wa vijiji wa Mengistu. Wakulima walipoteza uhuru wao, na nchi ilichukua ardhi yao na kudai mazao yao, yote haya kwa msaada na baraka za Benki ya Dunia. Katika miaka michache tu, Nyerere aligeuza nchi yake kuwa gofu, taifa la waombaji. Lakini Benki hii haijawahi kukubali makosa haya[9].

Katika muziki hariri

Muziki wa hip hop nchini Tanzania ulipata msukumo kutokana na mawazo na mandhari ya Ujamaa. Mwaka 1967, baada ya Rais Nyerere kuanzisha itikadi mpya ya siasa, ambayo aliahidi itawakomboa Watanzania kutoka ubeberu wa kimataifa, ilitelekezwa na wanasiasa wa Tanzania, kanuni za Ujamaa zilifufuliwa tena kupitia "njia isiyotarajiwa: Wanamuziki wa Rap na wasanii wa hip hop katika mitaa ya Tanzania[10].

Kama jawabu kwa miaka ya viongozi wafisadi wa serikali na wanasiasa baada ya Nyerere, dhana za umoja na familia na usawa zilikuwa ndio ujumbe uliotumwa katika muziki uliokuwa unatayarishwa. Hii ilikuwa kama mwitikio wa darasa la wafanyakazi katika mtazamo fulani ilikuwa upinzani.[11]Kanuni za uchumi wa ushirika -"wananchi wa kawaida kushirikiana ili kujipatia mahitaji muhimu ya maisha" - [12] ni maneno yanayoweza kuonekana katika nyimbo nyingi za hip hop za wasanii wa Tanzania. Zinapigia upatu ukuzaji wa biashara na kujitegemea katika jitihada za kuinua mioyo ya vijana na kuhamasisha mabadiliko katika jamii.

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 Pratt, Cranford (1999). "Julius Nyerere: Reflections on the Legacy of his Socialism". Canadian Journal of African Studies 33 (1): 137 – 52. doi:10.2307/486390. 
  2. Colin Legum, G. R. V. Mmari. Mwalimu: the influence of Nyerere. 
  3. Martin Plaut, "Africa's bright future", BBC News Magazine, 2 November 2012.
  4. David Edward O'Connor. The basics of economics. p. 100. 
  5. Colin Legum, G. R. V. Mmari (1995). Mwalimu: the influence of Nyerere. 
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 6.5 6.6 Challenging nature: local knowledge, agroscience, and food security in Tanga. Philip Wayland Porter. 
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 Rick Stapenhurst, Sahr John Kpundeh. Curbing corruption: toward a model for building national integrity. p. 153–156. 
  8. [24] ^ [https: / / www.policyarchive.org/bitstream/handle/10207/9616/89356_1.pdf?sequence=1 Tanzania's travail: Lessons in improving American aid to the Third World]
  9. Deressa, Yonas. Subsidizing tragedy: The World Bank and the new colonialism.[dead link]
  10. Lemelle, Sidney J. "'Ni Wapi tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha. " In the Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  11. Lemelle, Sidney J. "'Ni Wapi tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha. " In The Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  12. [27] ^ Denied: 1up! Archived 7 Julai 2011 at the Wayback Machine.Software Archived 7 Julai 2011 at the Wayback Machine.

Azimio la Arusha hariri

  • TANU, Dar es Salaam. (1967). The Arusha Declaration and TANU’s Policy on Socialism and Self Reliance. Dar es Salaam:Tanzania. Published by the Publicity Section, TANU, Dar es Salaam.

Machapisho ya mwl. Julius K. Nyerere kuhusu siasa hariri

  • Freedom and Unity (Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford University Press, 1967)
  • Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
    • Ndamo zimo: "The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance"; "The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and "Socialism and development."
  • Freedom & Development (Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford University Press, 1974)
    • Ndani zimo mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi ya uhuru.
  • Ujamaa - Essays on Socialism' (1977)
  • Crusade for Liberation (1979)

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri