Basil Pesambili Mramba
Basil Pesambili Mramba (15 Mei 1940 - 17 Agosti 2021) alikuwa mbunge wa jimbo la Rombo katika bunge la kitaifa nchini Tanzania.[1] Alikuwa anatokea katika chama cha CCM.
Miaka 1995-2000 alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, na pia mbunge. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo tangu 1980 hadi 1987 na tena kuanzia mwaka 1995 akaendelea kurudi bungeni hadi mwaka 2015.
Aliporudi bungeni mwaka 1995 aliteuliwa na rais Benjamin William Mkapa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, lakini alibadilishwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya hadi mwaka 2000. Baada ya kurudi bungeni alikuwa Waziri wa Fedha kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2005. Mwaka 2006, aliteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu, na mwaka huohuo alipelekwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko hadi mwaka 2008.[2].
Mwaka 2015 alihukumiwa kwenda jela miaka 3 katika kashfa ya mikataba ya ukaguzi wa dhahabu[3] pamoja na aliyewahi kuwa waziri wa nishati, Daniel Yona kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia taifa hasara ya Tsh bilioni 11.7 ($ milioni 5). Baada ya miezi 6 aliweza kutoka gerezani akipewa kazi ya kijamii.
Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 81 kutokana na ugonjwa wa Covid-19.[4]
Tazama pia
Marejeo
- ↑ Mengi kuhusu Basil Pesambili Mramba Ilihifadhiwa 20 Mei 2012 kwenye Wayback Machine., tovuti ya afdevinfo.com ya 1 Februari 2007, iliangaliwa 11 Novemba 2011
- ↑ https://www.theeastafrican.co.ke/tea/news/east-africa/tanzania-ex-minister-basil-mramba-dies-3514346
- ↑ https://www.reuters.com/article/ozatp-uk-tanzania-corruption-idAFKCN0PH0KU20150707
- ↑ https://www.theeastafrican.co.ke/tea/news/east-africa/tanzania-ex-minister-basil-mramba-dies-3514346
Viungo vya Nje
- HISTORIA FUPI YA BASIL PESAMBILI MRAMBA Ilihifadhiwa 26 Agosti 2021 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Jfivetv.com, tar., 17.08.2021, iliangaliwa Agosti 2021
- Member of Parliament CV, tovuti ya bunge ya tanzania, Januari 2014, kupitia archive.org.
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |