Bastola ni silaha ya moto yenye kasiba fupi inayoshikwa kwa mkono mmoja tu. Teknolojia yake ni karibu sawa na ya bunduki isipokuwa ni ndogo.

Bastola
Bastola aina za revolver

Aina za bastola hariri

Kiasili bastola ilikuwa tu umbo dogo la gobori. Baada ya kila pigo ilihitaji kujazwa upya.

Kwa muda bastola zenye kasiba mbili au zaidi zilitengenezwa kwa kusudi la kuongeza kasi ya kufyatulia risasi.

Baada ya kupatikana kwa ramia za metali katika karne ya 19 bastola ilipewa chemba ya risasi inayozunguka. Modeli mashuhuri ya mwanzoni ilikuwa aina ya Colt. Kwa Kiingereza aina hii huitwa "revolver" kutokana na mzunguko wa chemba. Chemba huwa na ramia 5-8, mara nyingi ni sita.

Aina ya pili kati ya bastola ina chemba ya risasi kama kidawati kidogo inayosukumwa ndani ya nafasi yake kwenye bastola. Wanajeshi waliona faida ya kwamba ni rahisi kujaza chemba ya ziada na kuibeba kama akiba inayobadilishwa haraka kuliko kujaza upya chemba inayozunguka kwa sababu chemba ya kuzunguka haitolewi, ni lazima kuijaza ramia moja-moja.

Matumizi ya bastola na bunduki hariri

Faida yake kulingana na bunduki yenyewe ni kuwa nyepesi na ndogo, hivyo haisumbui wakati wa kubeba. Hasara yake katika ulinganisho na bunduki ni hasa mfiko mdogo, nguvu ya risasi zake na umakinifu wa kulenga.

Jeshini bastola hutumiwa kama silaha ya pili pamoja na bunduki. Kwa polisi huwa ni silaha kali ya kawaida. Majambazi mara nyingi hupendelea bastola kwa sababu zinafichwa rahisi hazionekani.