Al Bayda au Beida (kwa Kiar. البيضاء ) ni mji mkubwa wa nne nchini Libya[1][2] na mji mkubwa wa pili katika sehemu ya mashariki baada ya Benghazi. Mwaka 2020 ilikuwa na wakazi 250,000[3].

Mahali pa Al Bayda katika ramani ya Libya
Msongamano wa magari katika Al Bayda

Ilikuwa makao makuu ya serikali wakati wa Ufalme wa Libya hadi mwaka 1969.

HistoriaEdit

Mji huu ulianzishwa kama mji wa Kigiriki miaka 2000 iliyopita[4]; jina la kisasa limetokea katika karne ya 19 wakati harakati ya Wasenussi walijenga chuo kikubwa (zawiyya) kwenye mlima juu ya mji; kutokana na rangi yake nyeupe mji wote ulianza kuitwa "zawiyya al-baida" na hatimaye "Al-Baida" pekee[5].

MarejeoEdit

  1. Libya Cyrene to re-enchant (fr). Libération (April 30, 2011). Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-05-14. Iliwekwa mnamo 2021-11-30.
  2. Libya Russian fears, Drogba & Libyan rebels. ESPNsoccernet (September 10, 2011). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-11-02. Iliwekwa mnamo 2021-12-26.
  3. Shahid, Anthony. "Free of Qaddafi, a City Tries to Build a New Order", The New York Times, March 6, 2011. 
  4. Cyrenaica and the Late Antique Economy Oxford University Computing Services. Retrieved 28 September 2011.
  5. Azema, James (2000). Libya Handbook: The Travel Guide. Footprint, 164. ISBN 978-1-900949-77-4. 

Viungo vya njeEdit