Belva Davis

Mwandishi wa Habari wa Runinga


Belva Davis (jina la kuzaliwa Belvagene Melton, Monroe, Louisiana, 13 Oktoba 1932) ni mwandishi wa habari wa redio na televisheni wa Kimarekani; ni mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuwa mwandishi wa habari katika televisheni ya West Coast ya Marekani. Ameshinda tuzo nane na ametambuliwa na Wanawake wa Amerika katika Redio na Televisheni na Chama cha Kitaifa cha Wanahabari Weusi.

Belvagene Melton
Amezaliwa 13 Oktoba 1932 (1932-10-13) (umri 92)
Monroe, Louisiana, United States
Nchi Marekani
Majina mengine Belva Davis
Kazi yake Mwandishi


Baada ya kukua katika mji wa Oakland, California, Davis alianza kuandika makala za kujitegemea katika majarida mnamo mwaka 1957. Ndani ya miaka michache, alianza kuripoti kwenye redio na televisheni. Kama mwandishi.Davis aliongoza hafla nyingi muhimu za siku, pamoja na masuala ya ubaguzi rangi, jinsia, na siasa. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuandaa kipidi chake mwenyewe cha mazungumzo kabla ya kustahafu mnamo mwaka 2012.

Maisha ya Awali

hariri

Belvagene Melton alizaliwa na Florence na John Melton ni mkubwa kati ya watoto wanne.[1][2]mama yake alikua na miaka minne alipokua anajifungua Belva,na Belva miaka yake ya mwanzoni ameisha na ndugu tofautitofauti.[3] Alipokuwa na umri wa miaka nane, Belva na familia yake, ikiwa ni pamoja na shangazi na binamu, walihamia kwenye nyumba ya vyumba viwili huko Oakland Magharibi kitongoji cha karibu na Oakland, California.watu kumi na moja waliishi katika ghorofa hiyo.[1] Baadaye Davis aliongea juu ya ujana wake na kusema , "Nilijifunza kuishi. Na nilipokuwa nikihama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine , nilijifunza kubadilika. Na wakati nilipokuwa mzee, niligundua kuwa ninaweza kuwa chochote kile ambacho ningehitaji kuwa."[3]

Mwishoni mwa miaka ya 1940, wazazi wake waliweza kumudu nyumba huko Berkeley, California. Davis alihitimu kutoka [[Berkeley High School (Berkeley, California) mnamo 1951, na kuwa mshiriki wa kwanza wa familia yake kuhitimu kutoka shule ya pili. Aliomba na kukubaliwa katika Chuo Kikuu cha Jimbo la San Francisco lakini hakuwa na uwezo wa kuhudhuria chuo kikuu.[4] SAlienda kufanya kazi kama mchapishaji huko Oakland Naval Supply Depot, akipata $2,000 kwa mwaka.[1]

Kazi ya uandishi wa habari

hariri

Davis alikubali kazi ya kujitegemea mnamo mwaka 1957 katika jarida la Jet,jarida linalozingatia maswala ya wamerakani weusi, na likawa la kwanza kwa uchapishaji. Alipokea $ 5 kwa kila kipande bila mstari. Kwa miaka michache baadae, alianza kuandika machapisho mengine ya Kiafrika pamoja na Amerika..

Maisha binafsi

hariri

Belva aliolewa na Frank Davis mnamo Januari 1 mwaka 1952. Walijaliwa watoto wawili na mjukuu wa kike, Davisi alikutana na mume wake wa pili ,Bill Moore mwaka 1967 alipokua anafanya kazi katika KPIX-TV.[1][5] Belva Davis, alikuwa ni mwanamke wa pekee katika redio pamoja na tv mbalimbali.

  • “Usiogope nafasi kati ya ndoto zako za ukweli. Ikiwa unaweza kuiota, unaweza kuifanya iwe hivyo. ” [6]

Heshima

hariri

Davis alishinda tuzo nane San Francisco.[7] Yeye ni mwanachama wa heshima wa Alpha Kappa Alpha.[8] Amepokea tuzo za mafanikio ya maisha kutoka kwa Wanawake wa Amerika katika Redio na Televisheni na Chama cha Kitaifa cha Wanahabari Weusi.[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Jones, Carolyn. "Belva Davis, grande dame of Bay Area journalism", May 9, 2010. Retrieved on November 14, 2012. 
  2. Guthrie, Julian. "Newswoman Belva Davis reflects on her life", January 20, 2011. Retrieved on January 7, 2013. 
  3. 3.0 3.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named mercury
  4. Harris, Janelle (Julai 30, 2014). "SO WHAT DO YOU, DO BELVA DAVIS, PIONEERING BROADCAST JOURNALIST, TV HOST AND AUTHOR?". Mediabistro. Iliwekwa mnamo Oktoba 15, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. De La O, Jessie (Mei 15, 2012). "Bay Area Journalist gives inspiring lecture". The Oak Leaf. Santa Rosa, California. Iliwekwa mnamo Januari 7, 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Holman Parmer, Janet. "Finding a Personal Side to the Homeless Story: Journalists Find a Cause in Petaluma", December 8, 1999. Retrieved on January 7, 2013. Archived from the original on 2018-07-13.  Kigezo:Subscription required
  6. https://www.goodreads.com/quotes/129983-don-t-be- fear-of-the-space-between-your-dreams-and
  7. Asimov, Nanette. "Groundbreaking journalist Belva Davis to retire", February 23, 2012. Retrieved on November 14, 2012. 
  8. "Membership: Honorary Members". Alpha Kappa Alpha Sorority, Incorporated. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 28, 2007. Iliwekwa mnamo Oktoba 12, 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Belva Davis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.