Firenze

(Elekezwa kutoka Florence)


Firenze (kwa Kiingereza Florence) ni mji katika Italia ya Kati na makao makuu ya mkoa wa Toscana. Kati ya mwaka 1865 hadi 1870 ilikuwa pia mji mkuu wa Ufalme wa Italia.

Firenze
Firenze is located in Italia
Firenze
Firenze

Mahali pa Firenze katika Italia

Majiranukta: 43°47′00″N 11°15′00″E / 43.78333°N 11.25000°E / 43.78333; 11.25000
Nchi Italia
Mkoa Toscana
Wilaya Firenze
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 360,000
Tovuti:  http://www.comune.fi.it/
Mji wa Firenze

Mji uko juu ya mto Arno. Idadi ya wakazi ni mnamo 360,000 na pamoja na rundiko la mji ni takriban 1,100,000.

Historia

hariri

Katika karne za kati Firenze ilikuwa kituo muhimu cha biashara, uchumi na utamaduni kwa Ulaya nzima. Kwa mfano, ni kati ya miji ambako uchumi wa benki ulijitokeza.

Firenze hutajwa mara nyingi kama chanzo cha kipindi cha "Renaissance" yaani kuzaliwa upya kwa ustaarabu wa kale wa Ulaya. Wakati ule ulitawaliwa na familia ya Medici. Mji umepambwa kwa majengo mazuri sana yaliyojaa picha za kupendeza. Wasanii wengi walio muhimu katika utamaduni wa Ulaya waliishi Firenze kama vile Donatello, Botticelli, Michelangelo na Leonardo da Vinci. Pia watu kama mwanafalsafa wa siasa Machiavelli, mpelelezi wa Amerika Amerigo Vespucci na mwanasayansi Galileo Galilei waliishi Firenze.

Sehemu ya mji imo katika orodha ya urithi wa dunia wa UNESCO.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Firenze kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.