Bernice Tlalane Mohapeloa

Bernice Tlalane Mohapeloa BEM (alizaliwa 1899 – amefariki 1997) alikuwa mwalimu na mwanaharakati kutoka Lesotho.

Maisha Ya Awali hariri

Bernice alizaliwa huko Nee Morolong Mafeteng, alipata elimu yake ya msingi huko, na kufaulu mitihani yake ya darasa la sita mwaka 1913. [1]

Kazi hariri

Mnamo 1943 Bernice alianza kufundisha katika Shule ya Upili huko Basutoland.[2].Kufikia mwaka 1944 Bernice alianzisha Chama cha Wahudumu wa Nyumbani cha Basutoland, kilichoundwa kufanana na vilabu, kama vile Klabu ya Uboreshaji wa Nyumbani katika Chuo Kikuu cha Fort Hare, ambacho alikuwa amekutana nacho Afrika Kusini.

Heshima na kutambuliwa hariri

Kwa hili, Bernice alipokea Medali ya himaya ya Uingereza katika Heshima za Siku ya Kuzaliwa mwaka 1946,katika mwaka huo huo bernice alikuwa mwanamke wa kwanza Mwafrika kupokea Ushirika wa Dorothy Cadbury.[3]

Marejeo hariri

  1. Scott Rosenberg; Richard F. Weisfelder. Historical Dictionary of Lesotho. Scarecrow Press. ku. 540–. ISBN 978-0-8108-7982-9. 
  2. David Ambrose (2007). The history of education in Lesotho: six brief subsectoral studies. House 9 Publications, National University of Lesotho. ISBN 978-99911-37-39-1. 
  3. The Delta Kappa Gamma Bulletin. Delta Kappa Gamma Society. 1962.