Bill McKibben

Mwanamazingira wa Marekani na mwandishi

'

Bill McKibben
Bill McKibben (2016)
Amezaliwa8 Desemba 1960
Kazi yakemwanamazingira, mwandishi, na mwanahabari wa nchini Marekani


William Ernest McKibben (alizaliwa 8 Desemba 1960) [1] ni mwanamazingira, mwandishi, na mwanahabari wa nchini Marekani ambaye ameandika kwa mapana juu ya athari za ongezeko la joto duniani. Pia ni Mwanazuoni mashuhuri wa Schumann katika Chuo cha Middlebury na kiongozi wa kampeni ya hali ya hewa katika shirika la 350.org. Ameandika vitabu kadhaa kuhusu mazingira, ikiwa ni pamoja na The end of Nature (1989), kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na Falter: Has the Human Game Begun to Play Itself Out? (2019) kuhusu hali ya changamoto za kimazingira zinazowakabili wanadamu na matarajio ya siku zijazo.[2]

Mnamo 2010, McKibben na shirika la 350.org walianzisha chama cha 10/10/10, ambacho kiliitisha zaidi ya matukio 7,000 katika nchi 188 duniani kote, [3][4] [5]kama alivyokuwa ameuambia mkutano mkubwa katika Chuo cha Warren Wilson muda mfupi kabla ya tukio. Mnamo Disemba 2010, 350.org iliratibu mradi wa sanaa wa kiwango cha sayari, na kazi nyingi kati ya 20 zikionekana kwa satelaiti.[6]

Marejeo

hariri
  1. "Bill Ernest McKibben." Environmental Encyclopedia. Edited by Deirdre S. Blanchfield. Farmington Hills, Mich.: Gale, 2009. Retrieved via Biography in Context database, December 31, 2017.
  2. McKibben, Bill (2019). Falter: Has the Human Game Begun to Play Itself Out? Description & arrow/scrollable preview. Henry Holt and Co. Retrieved 2022-03-07.
  3. "Deutscher Bundestag - Jamila Schäfer".
  4. Revkin, Andrew C.. "A Global Warming 'Work Party'", The New York Times, October 10, 2010. 
  5. "Global Work Party: 10/10/10 day of climate action". The Guardian. theguardian.com. October 11, 2010. Retrieved December 31, 2017.
  6. Revkin, Andrew C.. "Art on the Scale of the Climate Challenge", The New York Times, November 23, 2010. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bill McKibben kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.