Abimbola Rosemary "Bimbo" Odukoya (nee Abimbola Rosemary Williams; mara nyingi aliitwa "Mchungaji Bims," [1]; 12 Septemba 1960 - 11 Desemba 2005) alikuwa mchungaji na mhubiri wa runinga kutoka Nigeria ambaye alikuwa ameolewa na mwanzilishi wa Kanisa la chemchemi ya uzima, Taiwo Odukoya.

Odukoya alipokea zaidi ya tuzo 60 kitaifa na kimataifa kwa mchango wake wa ujenzi wa taifa, maendeleo ya nchi yake, Nigeria, na kanda ndogo ya Afrika Magharibi, na kwa uongozi kama mwanamke wa kiwango cha maadili na mfano wa kuigwa na wengi Kma mwandishi, mwinjilisti wa runinga maaarufu, msemaji katika mikutano ya kiwango cha juu,mshauriwa vijana na mshauri wa ndoa, alikuwa mmoja wa watu kadhaa waliochaguliwa kwa Samsung kuwakilisha Nigeria katika kubeba mwenge wa Olimpiki mjini Athens, Ugiriki katika 2004 Olympic Games. [2]

Maisha hariri

Odukoya alisoma Historia na Akiolojia katika Chuo Kikuu cha Ibadan ambapo yeye alpipata shahada ya Sanaa . Mchungaji Bimbo alifunga ndoa na Mchungaji mwanzilishaji wa Kanisa la chemchemi ya uzima, Mchungaji Taiwo Odukoya, na wakapata watoto watatu.

Alianza kazi yake kwenye jumba la taifa la usanii mjini Lagos na muda mfupi baadaye kujiuzulu na kuwa mchungaji wa kila saa. Kutoka 1987-1999, yeye aliwahi kuwa mkuu wa idara ya ushauri katika TREM chini ya uongozi wa Askofu Mike Okonkwo.

Wakati wa kifo chake, alikuwa mchungaji mkuu mwandamizi katika kanisa la chemchemi ya uzima na Rais wa Ugunduzi kwa Wanawake.

Alikuwa mwenyeji wa hawajaolewa na walioolewa, kipindi cha televisheni kilichoonyeshwa nchini na kimataifa ambacho kilihusika na masuala ya watu wanayokabili katika mahusiano ya ndoa na kuongozwa na kanuni za kibiblia. Alijulikana kama msemaji mashuhuri katika mkutano nchini Nigeria na wakati mwingine kiwango cha kimataifa.

Kifo hariri

Bimbo Odukoya alipanda ndege ya Kampuni ya huduma za ndege ya Sosoliso nambari 1145 iliyokuwa ikisafiri Bhari Harcourt kutoka Abuja. Tarehe 10 december 2005 ndege hyo ilipata ajali wakati ilipokuwa ikishuka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bahari Harcourt; Bimbo alinusurika matokeo ya awali na alikufa kutokana na majeraha tarehe 11 Desemba 2005. [1]

Vitabu Alivyoandika hariri

  • Jinsi ya kuchagua Mwenzako wa Maisha , na Bimbo Odukoya, "xulon Press (15 Oktoba 2005)
  • Kuishi Huru, kutatua vikwazo na Bimbo Odukoya, Wachapishaji wa Grace Spings , Inc, 2006
  • Kuishi Huru, Kutatua shida ya Kujisaga na Bimbo Odukoya,Wachapishaji wa Grace Springs , Inc, 2006
  • Maisha ya binafsi, Watu wa Kweli, Masuala ya Kweli ,Shauri la hekima na Bimbo Odukoya,Wachapishaji Grace Springs , Inc, 2006

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named ActofGod
  2. Ajimotokan, mile. "Odukoya, Bassey ni Olympic Torch Bearers." Archived 18 Januari 2005 at the Wayback Machine. Siku hii. 9 Julai 2004. Rudishwa tarehe 17 juni 2009.

Viungo vya nje hariri