Myombo
Myombo (Brachystegia spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Myombo wa Boehm (B. boehmii)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Miyombo ni aina za miti inayoitwa na wanabiolojia kwa jina Brachystegia. Jina la Kiswahili linatoka wingi wa jina la Kibemba: "muombo (miombo)", lakini kwa sababu fulani wingi huu umekuwa umoja kwa Kiswahili: "myombo (miyombo)".
Miti hii inaunda misitu isiyo minene hasa katika mazingira makavu kiasi ya Afrika ya Mashariki na Kusini hasa katika nchi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Angola, Tanzania na Malawi. Misitu ya miyombo inafunika maeneo ya kilomita za mraba milioni 5.
Misitu ya miyombo humwaga majani wakati wa majira ya ukame kwa kusudi la kuhifadhi maji ndani yao. Kabla ya kuja kwa majira ya mvua huotesha majani mapya. Wakati wa mabadiliko haya majani yanaonyesha rangi za dhahabu na nyekundu zinazopendeza.
Miyombo inayopatikana mara nyingi ni hasa Brachystegia boehmii na B. longifolia.[1]
Miyombo na watu
haririMisitu ya miyombo ni muhimu kwa maisha ya watu wanaoishi karibu nayo wakivuna hapa matunda, asali, kuni na lishe kwa mifugo. Kukatwa kwa miti hii imezidi kutokana na kuongezeka kwa watu na matumizi ya kuni. Utengenezaji wa makaa karibu na barabara kubwa yanayopelekwa mjini ni sababu muhimu. Katika maeneo ambako tumbako hulimwa wakulima wanakata miti mingi mno wakitumia kuni kukausha majani ya tumbako.
Wanyama
haririMiyombo inaota kwenye ardhi isiyo na rutba sana. Hata hivyo misitu ya miyombo ni nyumbani kwa spishi nyingi za wanyama pamoja na ndege wanaoishi hapa pekee. Wanyamapori wengi wanapata kinga na lishe kati ya miti hii kama vile tembo, mbwa mwitu, na wengine.
Spishi
hariri- Brachystegia allenii
- Brachystegia angustistipulata
- Brachystegia bakeriana
- Brachystegia bequaertii
- Brachystegia boehmii
- Brachystegia bussei, Mnyombo
- Brachystegia cynometroides
- Brachystegia eurycoma
- Brachystegia floribunda
- Brachystegia glaberrima
- Brachystegia glaucescens, Muunze
- Brachystegia gossweileri
- Brachystegia kalongensis
- Brachystegia kennedyi
- Brachystegia laurentii
- Brachystegia leonensis
- Brachystegia longifolia
- Brachystegia luishiensis
- Brachystegia lujae
- Brachystegia manga
- Brachystegia microphylla
- Brachystegia mildbraedii
- Brachystegia nigerica
- Brachystegia puberula
- Brachystegia russelliae
- Brachystegia spiciformis, Mrihi (mriti, msasa?, mtondo, mtondoro, mtundu, mundu)
- Brachystegia stipulata
- Brachystegia subfalcato
- Brachystegia tamarindoides, Mseni
- Brachystegia taxifolia
- Brachystegia torrei
- Brachystegia utilis
- Brachystegia wangermeeana
- Brachystegia zenkeri
Picha
hariri-
Muunze
-
Msitu wa miyombo katika kaskazini kwa tambarare ya Nyika, Malawi
Marejeo na Viungo vya Nje
hariri- ↑ Smith, Paul & Allen, Quentin: Field Guide to the Trees and Shrubs of the Miombo Woodlands, Royal Botanic Gardens, Kew 2004.
- Bruce M Campbell. ed. 1996. The Miombo Transition: Woodlands & Welfare in Africa, CIFOR, ISBN 9798764072, standard reference on the description & uses to which animals and man put these savanna woodlands.
- http://earthtrends.wri.org/text/forests-grasslands-drylands/map-234.html Ilihifadhiwa 19 Novemba 2004 kwenye Wayback Machine.
- Eastern Miombo woodlands (World Wildlife Fund)