Buibui-kofia
Aina ya buibui-kofia (Cryptocellus goodnighti)
Aina ya buibui-kofia (Cryptocellus goodnighti)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Oda: Ricinulei
Familia: Ricinoididae
Ewing, 1929
Ngazi za chini

Jenasi 3; spishi 11 katika Afrika:

Buibui-kofia (kutoka kwa Kiing. hooded tickspider) ni arithropodi wa familia Ricinoididae, familia ya pekee ya oda Ricinulei katika ngeli Arachnida. Jina lao linatoka kwa aina ya “kofia” ambayo wanaweza kutumia ili kufunika kichwa, mdomo na kelisera (chelicerae). Kwa kawaida buibui-kofia wana urefu wa mm 5-10 na wanafanana na utitiri. Wataalamu wengine wanafikiri kwamba wadudu hawa wana mnasaba na utitiri, lakini wengine wanafikiri kwamba wana mnasaba na oda ya zamani ya Trigonotarbida iliyokwisha sasa. Kefalotoraksi (cephalothorax) na fumbatio zimeungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija kama kwa buibui. Lakini ukingo wa fumbatio unaingia katika kunjo la gamba (carapace). Wana miguu minane kama arakinida wengine lakini jozi ya pili ni mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Hawana macho lakini spishi za zamani zilikuwa nayo na spishi za kisasa bado zina sehemu za kuhisi nuru. Mwenendo wa buibui-kofia haujulikani sana lakini inaonekana kwamba hula arithropodi wadogo kuliko hawa wenyewe.

Spishi za Afrika hariri

  Makala hii kuhusu "Buibui-kofia" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili hooded tickspider kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni buibui-kofia.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.