Shoronjano

(Elekezwa kutoka Calamonastides)
Shoronjano
Shoronjano utosi-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea
Familia: Acrocephalidae (Ndege walio na mnasaba na shoro)
Salvin, 1882
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 8 za shoronjano:

Shoronjano ni ndege wadogo wa jenasi Arundinax, Calamonastides na Iduna katika familia Acrocephalidae. Spishi nyingine za familia hii zinaitwa shoro kwa ufupi. Ndege hawa wana rangi ya kahawa mgongoni na njano chini. Wanatokea misitu au mabwawa ya mafunjo (Shoronjano domo-jembamba) ya Afrika. Hula wadudu. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa majani na pengine vijiti. Tago la kibwirosagi domo-jembamba limefungika mabua ya mafunjo. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika hariri

Spishi za Eurasia hariri

Picha hariri