Carolyne Ekyarisiima

Mwanamke mjasiriamali na mwanasayansi

Carolyne Ekyarisiima alizaliwa 20 Juni 1986 (1986-06-20) (umri 38) ni mwanasayansi, mjasiriamali jamii na mfanyabiashara katika nyanja za TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano), Kilimo na Elimu. Anafahamika zaidi kwa kuwa mwasisi mwenza wa shirika lisilokuwa la kiserikali linaloitwa Apps and girls ambalo lilianziswha likiwa na malengo ya kuongeza idadi ya wanawake katika fani ya sayansi kupitia TEHAMA kwa namna ya pekee kabisa ambapo mabinti wanapewa mafunzo ya kutengeneza programu za kompyuta sambamba na Ujasiriamali jamii (Tech Entreprenuership). Kupitia mafunzo hayo wanafunzi wanatengeneza miradi ya kusaidia jamii zao lakini pia kuanzisha biashara kwa malengo ya kuongeza nafasi za ajira na kupunguza umaskini katika Jamii.

Carolyne Ekyarisiima
Carolyne Ekyarisiima (2020)
AmezaliwaCarolyne Ekyarisiima
20 Juni 1986 (1986-06-20) (umri 38)
UraiaMganda
ElimuBweranyangi Girls' Senior Secondary School

Valley College Senior Secondary School
Kampala International University (CS) - Main Campus -Uganda

Kampala International University in Tanzania - KIUT (MIS)
Miaka ya kazi2014 - Mpaka Leo
Anajulikana kwa ajili yaMwanzilishi Apps and Girls Foundation
Mwanzilishi Mwenza WRIS Microfinance
Mwanzilishi WRIS Agro
Mwanzilishi Mwenza NLab Innovation Academy
Kazi maarufuMkurugenzi Mkuu, Mwanasayansi, Mfanya Biashara
NyumbaniDar es salaam, Tanzania
CheoCEO
Mwanachama bodi yaTangible Initiatives for Local Development Tanzania (TIFLD)
Tovuti
awww.appsandgirls.com

Maisha yake

hariri

Alizaliwa wilayani Bushenyi nchini Uganda katika familia ya watoto saba yeye akiwa wa tano. Akiwa mtoto alitamani sana kuwa Daktari wa kutibu binadamu lakini hakupata nafasi hiyo hasa baada ya hali ya uchumi kuyumba kidogo kutokana na kuwa na ndugu ambao nao walitakiwa kuendelea na elimu kwani Baba mzazi alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi na mama mzazi alikuwa ni mama wa nyumbani ilhali wazazi hawa walipenda sana watoto wao wote walau wafike kidato cha sita.

Udaktari ulikuwa ni gharama kubwa lakini kwa bahati akapata nafasi ya kusomea Computer Science katika Chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala kilichopo nchini Uganda na nihapo ndipo alipo anza kuutizama ulimwengu kivingine.

Katika Moja ya Mahojiano yake na waandishi wa habari anasema "Nikiwa KIU, Nikajikuta naanza penda Kozi niliyo chaguliwa ambayo ndio kwanza niliisikia nilipo ambiwa nimechaguliwa. Sikuwahi hata siku moja fikiria au waza juu ya Computer kuwa sehemu ya maisha yangu."[1]

Zaidi ya Kuwa Mkufunzi msaidizi, katika muda wake binafsi 2010 Carolyne alikuwa akishiriki katika kuanzishwa kwa OUFLab (Moja ya Hatamizi binafsi za mwanzo kabisa kuanzishwa nchini Tanzania) iliyo badilishwa jina mwaka 2013 na kuitwa NLab (Niwezeshe Lab) na baadaye kuja kuwa Chuo chenye kutoa stashahada na astashahada. Ushiriki huu ulihusisha mambo mengi kama Kuandaa semina za bure na wazi mashuleni na vyuoni, kuanzisha Program za "Friday Night Code" ambapo wanafunzi mbali mbali walijumuika kutoka Vyuo vikuu mbali mbali siku ya Ijumaa Jioni na kuanza kujifunza Coding mpaka Jumamosi Asubuhi na kwenda majumbani kwao, na haya yalifanyika huko Gongo La Mboto jijii Dar Es Salaam.

Mwaka 2012 mipango ya kuanza harambee ya kuiwezesha OUFLab[2] kununua vifaa ikaanza. Carolyne alishiriki kikamilifu katika mchakato huu, na kila hatua ilionesha namna ushiriki wa wanawake ulivyo wa kiwango cha chini. Mafunzo yaliyo fanyika katika Program zote za OUFLab yalihusisha wanawake na mabinti wachache. Mwaka 2013 Carolyne akashiriki mashindano Kadhaa yaliyo andaliwa na wadau mbali mbali wakiwemo TANZICT, COSTEC na DTBI. Moja ya mashindano hayo ni "Masoko Challenge[3]" iliyo fanyika Jully 1, 2013 ambapo Carolyne, Wilhelm na Geofrey kutoka OUFLab walishika nafasi ya Pili.

Baada ya mashindano Carolyne akaona kuna haja ya kile alicho kianza taratibu Nyumbani kwake kukifanya kiwe na ukubwa na hivyo Jully 26, 2013 akafanya mafunzo makubwa yaliyo husisha washiriki zaidi ya 30 kutoka vyuoni na makazini. Mafunzo haya yalikuwa na mafanikio makubwa sana[4]. Mwaka huo

Elimu yake

hariri

Carolyne alisoma nchini Uganda kuanzia elimu yake ya Awali mpaka kidato cha sita, na kisha kusoma chuo kikuu katika ngazi ya shahada ya sayansi ya kompyuta hapo hapo Uganda na baada ya kumaliza akapata ajira ya kudumu katika Chuo hicho na kuhamishiwa nchini Tanzania ambako nako akapata nafasi ya kuendelea kusoma na hivyo kusomea shahada ya uzamili ya mifumo ya habari (Information Systems) kutoka katika chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Tawi la Dar Es Salaam.[5]

Carolyne alianza kwa kufanya kazi katika chuo kikuu cha Kampala International University kilichopo jijini Dar es salaam, Nchini Tanzania. Aliajiriwa kama mkufunzi msaidizi. Mwaka 2013 Mwishoni aliacha kazi na kuanzisha Apps and Girls na yeye kuwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo.

Kupitia taasisi ya Apps and girls Carolyne anatoa elimu kwa njia ya

  • Kutoa mafunzo ya Computer Programming na Robotics kwa wanafunzi mashuleni, na hili analifanya kwa kutembelea mashule ya serikali na binafsi na kuanzisha Coding Clubs ambapo wanafunzi wanajiunga na kuweza anza jifunza pasipo malipo yoyote.
  • Anaandaa semina za kuamsha ari ya kupenda masomo ya sayansi na mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi waliopo katika shule za sekondari Tanzania Nzima.
  • Anaandaa Mashindano ya Kitaifa yaitwayo Girls Entreprenuership Summit ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakifadhiriwa na Ubalozi wa Marekani na pia Makampuni kama Tigo Tanzania na mengineyo.
  • Zaidi ya wanafunzi waliopo Mashuleni, wanamradi uitwao Jovia ambapo mabinti ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya secondary au chuo au kutokana na sababu za kupata ujauzito na kushinda kuendelea na shule, anawawezesha pia kwa kuwapa mafunzo ya Tehama na Ujasiriamali.

Wasichana wameweza kujifunza namna ya kutengeneza tovuti, programu za kwenye simujanja na huku baadhi wakianzisha taasisi za kusaidia jamii zao katika matatizo makubwa kama unyanyasaji na ukatili, kupunguza vio vya kina mama wakati wa kujifungua, kusaidia watu wenye magonjwa kama Fistula na Kansa na baadhi kuanzisha biashara kubwa zenye kuinua vipato vya familia zao.

Kubwa zaidi ni kwa mabinti hawa kuweza kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine katika jamii, na kupata fursa mbali mbali ambazo zimeweza kuwasaidia maishani na katika elimu zao. Baadhi ya wanafunzi wameweza kupata fursa za kimasomo na kuweza songa mbele huku taasisi nyingine zikijitokeza kuwasaidia zaidi na kutimiza ndoto zao. Kuna mabinto walio fanikiwa kusoma Biashara, Sheria, Sayanzi, Tehama, Uinjinia katika vyuo vikubwa duniani kama Oxxford na Rochester huku baadhi wakijiunga na masomo katika mashule na taasisi kubwa na Maarufu kama African Leadership Academy, African Leadership University , Anzisha Prize, [6] Baadhi ya wasichana ambao wameweza kupita katika mikono ya Carolyne Ekyarisiima ni Pamoja na Winnie Msamba, Balbina Gulam, Modesta Joseph, Necta Richard, Asha Abbas, Fatma Abbas, Lisa Jones, Ummy Bilinje, Elham Mohamed, Queen Mtega, Kokubanza Timanywa, Nancy Kaale na wengineo wengi ambao kwa namna moja ama nyingine nao wamepanda Mbegu ya maendeleo ndani ya Tanzania.

Biashara

hariri

Zaidi ya kuwa na mapenzi ya Teknolojia, Carolyne ni Mpenzi wa shughuri za kilimo na ufugaji. Anajishughurisha na biashara za Fedha, Kilimo cha mazao ya chakula na biashara , Biashara ya Vyakula, mifugo na wanyama.

Mijadala , Mihadhara na Mazungumzo

hariri
  1. Mkutano wa E-learning Afrika wa 2017 nchini Mauritius (Namna Teknolojia inavyo weza kutumika kama kitega uchumi katika kuwawezesha Mabinti na wanawake wa Africa) [7]
  2. Mkutano wa E-Learning Afrika wa Mwaka 2018 Nchini Rwanda (Kumwezesha mwanamke ni Utajiri mkubwa[8])

Tuzo na Teuzi mbalimbali

hariri

Kutokana na namna ya utendaji kazi wake binafsi na taasisi nzima ya Apps and Girls Carolyne akaweza kupata tuzo ndani na nje ya Tanzania ziki mpongeza yeye binafsi na Timu yake nzima.

  1. Tigo Digital Changemakers Award - 2017[9]
  2. Malkia wa Nguvu (2017) By Clouds Media Group
  3. The next generation of Leaders (2017) By IFA FOUNDATION [10]
  4. Innovator of the Year Award By Aid & International Development Forum
  5. 35 Most Influential Women in Tech By CIO Africa (Alitajwa)
  6. Digital Female Leader Awards (2019), Social Hero By Der DFLA (Aliteuliwa)
  7. 50 Most influential Young Tanzanians (2019) By Avance Media (Alitajwa)[11]

Marejeo

hariri
  1. "Apps and Girls win the Innovator of the Year Award | Health & WASH | Aid & International Development Forum (AIDF)". www.aidforum.org. Iliwekwa mnamo 2024-01-16.
  2. https://www.indiegogo.com/projects/community-owned-computer-lab-in-tanzania#/updates/all
  3. https://masokochallenge.wordpress.com/
  4. https://tanzict.wordpress.com/2013/07/17/joomla-training-for-women-26th-july-2013-8am-4-30pm/
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-19. Iliwekwa mnamo 2018-09-12.
  6. https://qz.com/africa/1214051/how-tanzania-is-betting-on-coding-to-help-close-the-gender-gap-in-its-tech-sector/
  7. https://avancemedia.org/2019miyt/
  8. https://www.elearning-africa.com/programme/pdf/eLA2018_programme.pdf
  9. "CAREER PROFILE : Bridging gender gap in technology". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-01. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
  10. "2017 Competition Winners | NextGen In Franchising". nextgenfranchising.org (kwa American English). 2018-02-21. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
  11. "Avance Media | Profiles: 2019 50 Most Influential Young Tanzanians" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.

Viungo vya nje

hariri
  1. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/woman/women-entrepreneurs-in-hi-tech-start-ups-2545326
  2. https://qz.com/africa/1214051/how-tanzania-is-betting-on-coding-to-help-close-the-gender-gap-in-its-tech-sector/
  3. http://www.aidforum.org/topics/health-and-wash/the-winner-of-the-innovator-of-the-year-award-is-announced/
  4. https://www.millicom.com/media/2808/final-tigo-digital-changemakers-sir-2015-regional-version.pdf
  5. https://www.s4ye.org/sites/default/files/2018-11/S4YE%20Digital%20Jobs%20Report.pdf
  6. https://docplayer.net/43764358-Africa-social-impact-report.html
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carolyne Ekyarisiima kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.