Simujanja

Simujanja ni aina ya simu ya mkononi ambayo inafanya mambo mengi kuliko simu nyingine.[1] Zinafanya kazi kama kompyuta lakini hii ni chombo kinachobebeka na kidogo cha kutosha katika mkono wa mtumiaji.

Simujanja zenye mfumo wa uendeshaji wa Android
Simujanja za Samsung
Simujanja imetumika kusoma Wikipedia
Toleo la simu ya kiganjani la HTC Desire Z, ikiwa na kioo kikubwa cha kugusa ikionesha baobonye ya QWERTY.

Matumizi yake ni pamoja na:

Kwa sababu simujanja ni kama kompyuta ndogo, zinaweza kuendeshwa kwa kutumia mifumo ya uendeshaji kama vile Apple iOS na Android - itategemea na mahitaji ya chombo chenyewe. Lakini vilevile wengine wanatumia Windows Phone au BlackBerry OS.[2]

HistoriaEdit

Simu ya kwanza kuuzwa ambayo inaweza kuitwa simujanja iliitwa "Angler": ilitengenezwa na Frank Canova mwaka 1992 wakati akifanya kazi IBM.[4][5][6]

Toleo lililoimarishwa zaidi liliuzwa mwaka 1994 na kampuni ya BellSouth kwa jina la Simon Personal Communicator. Pamoja na kupia na kupokea simu, simu hii iliweza pia kutuma nukushi na barua pepe. Simu hii ilikuwa na ramani, kalenda, kitabu cha namba za simu, saa, n.k.[7]

Neno "simujanja" halikutumika hadi mwaka mmoja baada ya kutolewa kwa simu hiyo.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  1. Andrew Nusca (20 August 2009). Smartphone vs. feature phone arms race heats up; which did you buy?. ZDNet.
  2. Smartphone definition from PC Magazine Encyclopedia. PC Magazine. Iliwekwa mnamo 13 May 2010.
  3. Watch The Incredible 70-Year Evolution Of The Cell Phone. Wonder How To. Iliwekwa mnamo March 5, 2015.
  4. Sager, Ira (June 29, 2012). Before IPhone and Android Came Simon, the First Smartphones. Bloomberg Businessweek. Bloomberg L.P. Iliwekwa mnamo June 30, 2012. “Simon was the first smartphone. Twenty years ago, it envisioned our app-happy mobile lives, squeezing the features of a cell phone, pager, fax machine, and computer into an 18-ounce black brick.”
  5. Schneidawind, John. "Poindexter putting finger on PC bugs; Big Blue unveiling", November 23, 1992, p. 2B. 
  6. World's first 'smartphone' celebrates 20 years. BBC News. Iliwekwa mnamo August 16, 2014.
  7. History of first touchscreen smartphone Archived Mei 1, 2016, at the Wayback Machine Spinfold.com