Catherine Ruge

Mwanasiasa wa Tanzania ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema (Viti Maalum) wa Serengeti, kati ya 2017 na 2020.

Catherine Ruge (alizaliwa Juni 25, 1982)[1] alikuwa mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya chama cha CHADEMA akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Macha aliyefariki dunia 21 Machi 2017.[2].

Alisoma Shule ya Sekondari Msalato mkoani Dodoma kuanzia mwaka 2001 hadi 2003. Baadaye alisoma Jangwani kuanzia Juni 2001 hadi Mei 2003 na kuhitimu elimu ya juu ya sekondari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2004 hadi 2007 akisomea Shahada ya Biashara na Uhasibu. Mwaka 20112015 alisoma Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara katika chuo cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute). Kwa sasa anachukua masomo ya udaktari (PHD) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye masuala ya jinsia katika fani ya uhasibu.[3]

Harakati za kisiasa

hariri

Alijiunga na Chadema mwaka 2010 na ilipofika mwaka 2013 mwishoni alianza rasmi harakati za siasa.Alianza kwa kugombea nafasi ya katibu wa rasilimali fedha Kanda ya Serengeti na kushinda.[4]

Tarehe 04 Mei, 2017 aliteuliwa na NEC kuwa Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya chama cha CHADEMA kwa kuchukua nafasi ya Dr Elly Marco Macha.[5] [6]<

Anasifika kwa michango yake adhimu bungeni, hasa katika nyanja za mazingira na haki za wanawake na watoto wa kike. Ni mwanamke wa kwanza katika kijiji hicho kumaliza kidato cha sita na kupata shahada ya Chuo Kikuu, shahada ya Uzamili na Uzamivu pia. Mwanaharakati huyu wa haki za binadamu alikataa kukeketwa kama ilivyokuwa jadi ya jamii katika usichana wake, vita anavyoviendesha mpaka hivi sasa kupinga unyanyasaji na ukeketaji. Kwa jitihada zake alijenga bweni la kisasa katika Sekondari ya Ring'wani kwa ajili ya watoto wa kike walio katika mazingira magumu, na anafahamika kwa kutoa misaada ya mahitaji maalumu katika shule za wilayani, hasa kwa watoto wanaotoka katika kaya masikini. Mbunge huyu kijana amevunja rekodi kwa kujenga nyumba ya kisasa zaidi ya orofa moja kijijini kwake Ring'wani.

Marejeo

hariri
  1. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Mbunge-mpya-Chadema-azungumzia-mikakati-yake/1597578-3916058-ohyr2mz/index.html
  2. https://www.ippmedia.com/sw/habari/ruge-ateuliwa-kuwa-mbunge
  3. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Mbunge-mpya-Chadema-azungumzia-mikakati-yake/1597578-3916058-ohyr2mz/index.html
  4. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Mbunge-mpya-Chadema-azungumzia-mikakati-yake/1597578-3916058-ohyr2mz/index.html
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-31. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  6. https://globalpublishers.co.tz/138922-2