Kuchamwamba
(Elekezwa kutoka Chaetopidae)
Kuchamwamba | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Kuchamwamba ni ndege wa jenasi Chaetops, jenasi pekee ya familia Chaetopidae, lakini spishi nyingine, kuchamwamba wa Damara, ni jamaa ya kucha wa Afrika. Spishi za Chaetops hazina mnasaba na kucha wengine bali na jamii ya kunguru.
Ndege hawa ni weusi wenye masharubu meupe na rangi ya machungwa au nyekundu kwa kidari, tumbo na kiuno. Mabawa yao ni mafupi kwa hivyo hawaruki angani sana lakini hukimbia na kurukia miwambani.
Wanatokea Afrika Kusini na Lesoto.
Hula wadudu hasa na mijusi, vyura, buibui, nge na nyungunyungu pia. Tago lao hujengwa kwa nyasi ardhini na jike hutaga mayai 2-3. Watoto wao wakubwa husaidia kutunza makinda.
Spishi
hariri- Chaetops aurantius, Kuchamwamba Kidari-machungwa (Drakensberg au Orange-breasted Rockjumper)
- Chaetops frenatus, Kuchamwamba Kidari-chekundu (Cape au Rufous Rockjumper)
- Achaetops pycnopygius, Kuchamwamba wa Damara (Damara Rockjumper au Rockrunner) – haina mnasaba na Chaetops lakini imo baina ya kucha wa Afrika
Picha
hariri-
Kuchamwamba kidari-machungwa
-
Kuchmwamba kidari-chekundu