Chuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz
Yıldız Teknik Üniversitesi (YTÜ, au YTU kwa lugha ya Kiingereza Chuo Kikuu cha ufundi cha Yildiz) ni chuo kikuu cha ufundi, wakfu ya sayansi na uhandisi na ni moja ya taasisi za elimu maarufu zaidi katika mji wa Istanbul, Uturuki. Chuo hicho kipo ndani ya wilaya Beşiktaş.
Chuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz | |
---|---|
Yıldız Teknik Üniversitesi | |
Walimu | 1384 |
Wanafunzi | 21,000 |
Mahali | {{{mji}}} |
Historia
haririChuo Kikuu cha Ufundi cha Yildiz kilianza 1911. YTU ilianzishwa kama Kondüktör Mekteb-i Âlisi / Shule ya Elimu ya Juu ili kuweza kukabiliana na mahitaji ya Manispaa ya Umma na Sehemu ya Kazi na kutoa huduma kwa "afisa wa sayansi" (waliojulikana awali kama conductors, na leo kama mafundi). Shule hiyo iliundwa ili ufwate mfumo wa elimu ya juu ya ufundi ya "École de Conducteur" na iliungwa na Wizara ya Kazi za Umma.
Jina la shule lilibadilishwa na kuitwa Nafia Fen Mektebi mwaka 1922 na muda wa elimu uliongezwa kutoka miaka 2,5 hadi miaka 3 kati ya mwaka 1926 na 1931.
Kufuatia kuongezeka kwa huduma za umma na mahitaji ya huduma za kiufundi, sheria mpya iliamuru kufungwa kwa Nafia Fen Mektebi na kuanzishwa kwa shule ya Ufundi ili kukabiliana na pengo lililokuwa kati ya maafisa wa kiufundi na wahandisi wa kitaaluma. shule hiyo ilikuwa na mpango wa miaka 2 kwa ajili ya maafisa wa kiufundi na mpango wa miaka 4 kwa ajili ya uhandisi na ulipewa baadhi ya majengo ya ukumbi wa Yildiz, ambayo bado yako katika matumizi hadi leo.
Katika vipindi vya mwanzo shule ilitoa elimu ya ujenzi na idara za mitambo ya sayansi ili kuelimisha wanafunzi kuwa walinzi wa kiufundi na wahandisi. Kati ya 1942-1943 idara ya usanifu na ya umeme zilianzishwa kama sehemu ya idara ya uhandisi. shule hiyo ilikubaliwa kama moja ya vyuo vya elimu ya juu na taasisi ya utafiti katika mwaka 1969. Mwaka 1971 sheria mpya ilitoa amri ya kufungwa kwa shule maalum za ufundi, vyuo vya uhandisi viliimarishwa na Jimbo la Uhandisi na chuo cha kimimari cha Istanbul.
Yildiz teknik Üniversitesi ilikubaliwa kama jina rasmi la shule mwaka 1992. Kitivo cha Uhandisi kiligawanywa katika vyuo vinne, Kitivo cha umeme, Kitivo cha Ujenzi, Kitivo cha Mitambo na Vyuma na Kitivo cha Sayansi ya Uchumi na Utawala. Kitivo cha Uhandisi cha Kocaeli na Shule ya Ufundi ya Kocaeli vilitengwa na chuo kikuu cha Yildiz na kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kocaeli. Leo YTU inatoa elimu katika vyuo vyake 9, taasisi 2, Shule ya Ufundi ya Elimu ya Juu na Shule ya Mafunzo ya Lugha za Nje kwa zaidi ya wanafunzi 17.000.
Vitivo
hariri- Kitivo cha Umeme na Kompyuta kurasa rasmi
- Kitivo cha Fasihi na Mafunzo ya Taifa ya Utamaduni
- Kitivo cha Sanaa na Sayansi
- Kitivo cha Elimu
- Kitivo cha Sayansi ya Uchumi na Utawala - kurasa rasmi
- Kitivo cha Ujenzi - kurasa rasmi
- Kitivo cha kemia
- Kitivo cha Uhandisi wa Mitambo - kurasa rasmi
- Kitivo cha Kimimari - kurasa rasmi Archived 14 Aprili 2011 at the Wayback Machine.
- Taasisi ya Sayansi na Uhandisi
- Taasisi ya Sayansi ya Jamii
- Shule ya Mafunzo ya Ufundi
- Shule ya Lugha ya Nje
Picha
hariri-
Mlango wa chuo -
jengo la Çukursaray -
Kitivo cha Mimari -
Jengo la A -
Jengo la YTU
-
Kampasi ya Davutpasa
-
Kampasi ya Besiktas
-
Kampasi ya Besiktas
-
Kampasi ya Besiktas
-
Maktaba
-
Kampasi ya Besiktas
-
Kampasi ya Besiktas
-
Kampasi ya Besiktas
-
Kampasi ya Davutpasa
-
Kampasi ya Davutpasa
-
Kampasi ya Davutpasa
-
Kampasi ya Davutpasa
Viungo vya nje
hariri- kurasa rasmi ya YTU Archived 6 Februari 2016 at the Wayback Machine. (Kituruki)
- http://www.yildiz.edu.tr/en/index.php Archived 6 Julai 2010 at the Wayback Machine.
- Alumni Archived 9 Oktoba 2021 at the Wayback Machine. (Kituruki)
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |