Conakry

mji mkuu wa Guinea


Conakry (pia: Konakry) ni mji mkuu wa Guinea wenye wakazi 2,000,000 (mwaka 2002). Mji una bandari mwambaoni wa Ghuba ya Guinea ya Atlantiki.

Jiji la Conakry
Nchi Guinea
Conakry katika Guinea.
Jumba la Watu mjini Conakry
Uwanja wa michezo Lansana Conte.

Historia

hariri

Chanzo cha Conakry ni kwenye kisiwa cha Tombo kilicho karibu sana na rasi ya Kaloum. Mji ulianzishwa baada ya kisiwa hicho kuhamishwa kutoka utawala wa Uingereza kwenda chini ya Ufaransa. Wafaransa waliunganisha mwaka 1887 vijiji vinne vya Conakry, Boulbinet, Krutown na Tombo. Mwaka 1889 Conakry ilikuwa makao makuu ya utawala wa koloni ya « Mito ya Kusini (Rivières du Sud) » na tangu 1891 ya Guinea ya Kifaransa ikakua kwa sababu ya bandari yake hasa baada ya kujengwa kwa reli kwenda Kankan.

Conakry leo

hariri

Leo kisiwa cha Tumbo kimeunganishwa na rasi ya Kaloum kwa barabara. Mji umeenea kufunika rasi yote. Kuna beledi tano mjini ambayo ni Kaloum (kitovu cha mji), Dixinn (penye chuo kikuu na balozi nyingi), Ratoma (penye vilabu na mabaa), Matam na Matoto penye uwanja wa ndege wa Gbessia.

Mahali pa kuangaliwa ni makumbusho ya kitaifa, masoko, jengo la Jumba la Watu, msikiti mkuu na visiwa vya Los.