Konfusio

(Elekezwa kutoka Confucius)

Konfusio (kwa Kichina: Kǒngzǐ (孔子) au Kǒng Fūzǐ (孔夫子) -- Mwalimu Kong) (551 KK - 479 KK) alikuwa mwalimu na mwanafalsafa muhimu kabisa wa kale huko Uchina.

Picha ya Konfusio

Jina halisi

hariri

Jina lake halisi lilikuwa Kong Qiu (kwa Kichina: 孔丘) au Zhong Ni (kwa Kichina: 仲尼).

Maisha

hariri

Alizaliwa katika Jimbo la Lu (魯), China mnamo 27 ya mwezi namba nane kwa kalenda ya Kichina (inayotegemea Mwezi) mwaka 551 KK. Baba yake alikuwa akiitwa Shu Liang He (叔梁纥), na mama yake alikuwa akiitwa Yan Zheng Zai (顏徵在).

Kuanzia umri wa miaka 3, baba yake alipofariki, akawa anaishi na mama yake.

Akiwa bwana mdogo, alikuwa na shauku hasa ya kijifunza mambo mengi, na alikuwa na mapenzi sana na masuala ya ibada.

Pindi alipokua, alifanyakazi kama mmiliki rasmi wa mashamba na ng'ombe, kisha akawa mwalimu.

Confucius aliishi kipindi ambacho majimbo mengi yalikuwa yakipigana vita nchini China. Kipindi hicho kilikuwa kikiitwa Bubujiko na Demani wakati wa kipindi cha Nasaba ya Zhou. Confucius hakulipenda hili na kutaka kurejesha hali ya kawaida katika jamii.

Athira kiutamaduni

hariri

Tarehe ya kuzaliwa ya Confucius (28 Septemba) ni sikukuu kule China. Katika siku hiyo watu husherekea walimu.

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Konfusio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.