Kurumbiza

(Elekezwa kutoka Copsychus)
Kurumbiza
Kurumbiza utosi-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
J. Fleming, 1822
Ngazi za chini

Jenasi 15:

Kurumbiza ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia ya Muscicapidae. Spishi nyingine zinaitwa madende. Zamani waliainishwa katika familia ya mikesha (Turdidae). Mkia wao ni mrefu kuliko ule wa zuwanende. Wana rangi ya kijivu, nyeusi, buluu au kahawa mgongoni na spishi nyingi wana koo na kidari ya rangi ya machungwa au nyekundu. Hawa ni ndege wa misitu ya Afrika na Asia. Madume ya spishi kadhaa waimba vizuri sana (k.m. Kurumbiza wa Ulaya). Hula wadudu hasa lakini spishi nyingine hula buibui, nyungunyungu na vyura na mijusi wadogo pia, na pengine hata beri. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika mti, kichaka au tundu ya asili. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri