Daraja la Dona Ana
Daraja la Dona Ana ni daraja linalovuka Mto Zambezi nchini Msumbiji kati za miji za Mutarara na Sena. Likiwa na urefu wa kilomita 3.7 ni daraja defu la kuvuka Zambezi. Lilijengwa mnamo 1934 zamani za ukoloni wa Kireno kwa mvuko wa reli kwa kusudi la usafiri kati ya Malawi, migodi ya makaa mawe ya Mutarara na bandari ya Beira.
Daraja la Dona Ana English: Dona Ana Bridge Kireno: Ponte Dona Ana | |
---|---|
Yabeba | Reli ya Sena |
Yavuka | Mto Zambezi |
Mahali | Vila de Sena, Msumbiji |
Mbunifu wa mradi | Edgar Cardoso |
Urefu | mita 3,670 |
Idadi ya nguzo | 40 |
Yatanguliwa na | Daraja la Samora Machel |
Yafuatiwa na | Daraja la Armando Emilio Guebuza |
Anwani ya kijiografia | 17°26′31″S 35°03′07″E / 17.44194°S 35.05194°E |
Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji daraja likaharibiwa na tangu 1995 kutengenezwa kwa usafiri wa magari. Tangu mwaka 2009 hutumiwa tena kwa usafiri wa reli.
Makala hii kuhusu daraja barani Afrika bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |