Dawa ya kibiolojia

(Elekezwa kutoka Dawa za kibiolojia)

Dawa ya kibiolojia ni dawa ya kudhibiti viumbehai wasumbufu au waharibifu ambayo ina viambato viasilia, k.m. vidubini au misindiko ya mimea. Dawa hizi huunda sehemu ya udhibiti wa kibiolojia pamoja na kuachia kwa wadudu wa kidusia au vidusia vyingine.

Fasiri zinatofautiana kati ya nchi, k.m.:

  • katika Ulaya dawa za kibiolojia hufasiriwa kama “aina za viuawadudu vilivyo na vidubini au vifundiro viasilia ndani yao”[1].
  • katika Marekani dawa hizi ni “maada asilia zinazodhibiti viharibifu (dawa za kibiokemikali), vidubini vinavyodhibiti viharibifu (dawa za vidubini) na maada viuawadudu zinazotolewa na mimea ambayo imepewa jeni za kigeni (vilinda vilivyoingizwa katika mimea)”[2].

Kwa kawaida zinategenezwa kwa kukuza na kukusanya vidubini vinavyotokea uasiliani, labda pamoja na vifundiro vya metaboli vyao, k.m. bakteria, virusi, kuvu na protozoa. Nematodi hushirikishwa katika orodha hii ijapokuwa si vidubini kwa kweli. Dawa hizi zinachukuliwa mara nyingi kama visehemu shiriki vya miradi ya mchanganyiko wa udhibiti wa viharibifu (Kiing.: integrated pest management) na zinatumika zaidi na zaidi badala ya dawa za kikemikali[3].

Maelezo

hariri

Kuna madaraja makubwa matatu ya dawa za kibiolojia:

  • Dawa za vidubini ambazo zina virusi viuawadudu, bakteria, kuvu viuawadudu, protozoa au nematodi viuawadudu ndani yao[4][5]. Kwa mfano, utumizi wa nematodi kama viuawadudu kukabiliana na mchwa.[6]
  • Dawa za kibiokemikali au za mitishamba ambazo zina misindiko ya mimea ndani yao[7].
  • Maada zinazolinda dhidi ya viharibifu na zinazotengenezwa na mimea ambayo imepewa jeni za kigeni (Kiing.: GM crops). Mimea kama hii inakatazwa katika nchi nyingi, katika Ulaya hasa.

Mifano ya vidubini vitumikavyo katika dawa za kibiolojia

hariri

Bacillus thuringiensis (Bt) anasababisha magonjwa katika vipepeo, mbu na mende-vibyongo. Dawa zenye Bt zinaitwa dawa za vidukini kwa kawaida lakini hii siyo sahihi kabisa kwa sababu wingi wa dawa hizi hazina bakteria hai ndani yao lakini fuwele za sumu zao tu. Jeni zilizo na kodi ya kutengeneza sumu hizi zimeingizwa katika mimea ipandwayo, k.m. mpamba, muhindi, kiazi cha kizungu na soya. Kwa hivyo mimea hii inaweza kuua viwavi na lava wa mende-vibyongo bila haja ya kupulizia dawa. Ingawa dawa zenye Bt na mimea yenye jeni za sumu za Bt hazina hatari kwa viumbehai vingine kuliko dawa za kikemikali, mgusano uliorudia au wa muda mrefu na sumu za Bt unaweza kusababisha mabadiliko ya kihistopatolojia katika ini na mafigo ya mamalia[8].

Dawa nyingi za vidubini zina kuvu viuawadudu ndani yao, kama spishi za Metarhizium, Beauveria, Isaria na Lecanicillium. Dawa hizi hazina haja ya kumezwa kwa sababu kuvu hizi zinapenya kiunzi nje cha wadudu. Kuna spishi nyingi za virusi zinazotumika katika dawa za vidubini, lakini ni lazima dawa hizi zimezwe. Kinyume na virusi na kuvu nematodi viuawadudu, kama spishi za Steinernema na Heterorhabditis, huingia wenyewe kupitia tundu yoyote ya kiwiliwili (kinywa, mkundu, spirakulo n.k.) lakini spishi kadhaa zinaweza kupenya kiunzi nje. Dawa za kudhibiti magonjwa ya mimea zina kuvu kama spishi za Trichoderma au bakteria kama spishi za Bacillus (B. subtilis hasa). Mwishowe kuna dawa za kiuamagugu zilizo na kuvu kama spishi za kuvu-kutu.

Dawa za kibiokemikali zinaweza kuwa na misindiko ya mimea iliyo na alkaloidi, terpenoidi na fenoli ndani yao. Mfano unaojulikana sana ni mafuta ya mwarobaini (Kiing.: neem oil). Dawa nyingine zina vifundiro vya kuchachuka kama Spinosad. Hata wadudu wanatengeneza molekuli ambayo zinaweza kutumika kama dawa, mahususi feromoni. Molekuli hizi haziui lakini zinatafiri kupandana kwa wadudu.

Utumiaji

hariri

Kwa kawaida dawa za kibiolojia hutumika kwa njia sawa kama dawa za kikemikali lakini namna za matendo ni tofauti na bila hatari kwa mazingira. Ili kufanya kazi vizuri ni lazima dawa hizi zichanganywe na viambato na vizimuo sadifu[9] na njia sadifu za kupulizia zitumike[10][11]. Hata hivyo, mara nyingi hali ya hewa ni ya maana, k.m. unyevuanga mkubwa.

  • Hakuna shida na mabaki juu ya mazao
  • Bei inaweza kuwa rahisi kuliko ile ya dawa za kikemikali, hususa zikizalishwa kieneo
  • Zinaweza kufanya kazi vyema kuliko dawa za kikemikali baada ya muda (Mradi wa LUBILOSA umeonyesha hii k.m.)
  • Zinayeyushwa na vidubini

Madhara

hariri
  • Zinaua spishi chache tu kuliko dawa za kikemikali, kwa hivyo masoko ni madogo kiasi (faidi ni kwamba dawa hizi haziui viumbehai wa manufaa kwa kawaida)
  • Namna ya tendo ni nzito, kwa hivyo haziwezi kutumika ambapo shamba limeshajaa na viharibifu
  • Zinategemea sana hali ya hewa (halijoto na unyevuanga)

Angalia pia

hariri

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri
  1. http://ec.europa.eu/environment/integration/research/newsalert/pdf/134na5.pdf Ilihifadhiwa 15 Mei 2012 kwenye Wayback Machine. European Commission (2008) Encouraging innovation in biopesticide development. Accessed on 20 April 2012
  2. http://www.epa.gov/opp00001/biopesticides/ Environmental Protection Agency of the USA (2012) Regulating Biopesticides. Accessed on 20 April 2012
  3. Copping L.G. (ed.) (2009). The Manual of Biocontrol Agents 4th Ed. British Crop Production Council (BCPC), Farnham, Surrey, UK; 851 pp. {{cite book}}: |author= has generic name (help)
  4. Coombs, Amy. "Fighting Microbes with Microbes". The Scientist. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Francis Borgio J, Sahayaraj K and Alper Susurluk I (eds) . Microbial Insecticides: Principles and Applications, Nova Publishers, USA. 492pp. ISBN 978-1-61209-223-2
  6. Ambru says (2018-11-24). "How to Get Rid of Termites: A Comprehensive Guide (2019)". PestsGuide (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-06-25.
  7. Pal, GK; Kumar, B (2013). "Antifungal activity of some common weed extracts against wilt causing fungi, Fusarium oxysporum" (PDF). Current Discovery. 2 (1). International Young Scientist Association for Applied Research and Development: 62–67. ISSN 2320-4400. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-12-16. Iliwekwa mnamo Februari 8, 2014. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)Kigezo:Open access
  8. Kiliç, A; Akay, M. T. (2008). "A three generation study with genetically modified Bt corn in rats: Biochemical and histopathological investigation". Food and Chemical Toxicology 46 (3): 1164–70.
  9. Burges, H.D. (ed.) 1998 Formulation of Microbial Biopesticides, beneficial microorganisms, nematodes and seed treatments Publ. Kluwer Academic, Dordrecht, 412 pp.
  10. Matthews GA, Bateman RP, Miller PCH (2014) Pesticide Application Methods (4th Edition), Chapter 16. Wiley, UK.
  11. L Lacey & H Kaya (eds.) (2007) Field Manual of Techniques in Invertebrate Pathology 2nd edition. Kluwer Academic, Dordrecht, NL.