Demetrius I wa Aleksandria

Demetrius I wa Aleksandria (alifariki 22 Oktoba 232) alikuwa Patriarki wa 12 wa jiji hilo la Misri lililowahi kuinjilishwa na Mtakatifu Marko.

Mt. Demetrius I wa Aleksandria.

Kabla ya hapo alikuwa mkulima na kuishi na mke na ndugu[1].

Klementi wa Aleksandria alipoacha kuongoza shule ya Aleksandria, Demetrius alimchagua kama mwandamizi wake kijana Origen, ila baadaye alimlaumu kwa kuhubiri akiwa mlei[2], tena kwa kupewa upadrisho bila idhini yake[3].

Demetrius aliongoza Kanisa miaka 42 akafa akiwa na umri wa miaka 105[4].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Oktoba[5].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • "Dimitrios (189–232)". Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Iliwekwa mnamo 2011-02-08.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.