Upadirisho

(Elekezwa kutoka Upadrisho)

Upadirisho ni sakramenti ya kumwekea wakfu mtu katika daraja ya upadri.

Katika upadirisho, baada ya askofu, mapadri wote waliopo wanawawekea mikono mashemasi. Hapo tu inafuata sala ya kuwaweka wakfu.

Kanisa Katoliki na Waorthodoksi wanauona kuwa wa lazima kabisa ili mtu aweze kutoa huduma za kasisi.

Kiini cha ibada hiyo ni Askofu kumwekea mikono kichwani shemasi na kutoa sala maalumu ya kumweka wakfu kwa daraja hiyo.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upadirisho kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.