Den Haag
Den Haag (Kiholanzi pia: 's-Gravenhage) mji mkubwa wa tatu wa Uholanzi baada ya Amsterdam na Rotterdam. Kuna wakazi 472,087 (1 Januari 2005) kwenye eneo la 100 km². Iko upande wa magharibi ya nchi katika jimbo la Uholanzi ya Kusini pia ni ,akao makuu ya jimbo hilo.
Mji mkuu hali halisi
haririHali halisi Den Haag ina nafasi na wajibu nyingi za mji mkuu hata kama cheo hiki kimetengwa kwa Amsterdam. Lakini Den Haag ni makao ya serikali, makao ya bunge, makao ya mahakama kuu pia makao ya mfalme au malkia tangu 1831. Balozi zote za nje ziko hapa pia.
Taasisi za Kimataifa
haririDen Haag ni makao ya taasisi 150 za kimataifa. Hii ni tokeo la siasa ya Uholanzi ya miaka mingi ya kutoshikamana na upande wowote.
Kati ya taasisi zinazojulikana zaidi ni:
Picha za Den Haag
hariri-
Bwawa mbele ya bunge
-
Hoftoren ni jengo kubwa la Den Haag
-
Manisipaa mpya
-
Nyumba za ghorofa kitovuni ya mji
Makala hii kuhusu maeneo ya Uholanzi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Den Haag kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |