Denny Vrandečić

mwanasayansi wa kompyuta wa Kroatia

'

Denny Vrandečić
Dr. Denny Vrandečić
Amezaliwa27 Februari 1978
Kazi yakemwanasayansi wa kompyuta


Zdenko "Denny" Vrandečić (alizaliwa Stuttgart, Ujerumani, 27 Februari 1978) ni mwanasayansi wa kompyuta kutoka Korasia.

Alikuwa msanidi mshirika wa Semantic MediaWiki na Wikidata, msanidi mkuu wa mradi wa Wikifunctions, na mfanyakazi wa Wikimedia Foundation akiwa kiongozi wa miradi maalum, na miradi iliyopangwa kufanyika mbeleni.[1] Alichapisha moduli katika mchezo wa kuigiza wa Kijerumani The Dark Eye.

Anaishi katika eneo la San Francisco Bay huko California, Marekani.[2]

Vrandečić alihudhuria shule ya upili ya Geschwister-Scholl huko Stuttgart na tangu mwaka 1997 alisomea sayansi ya kompyuta na falsafa katika Chuo Kikuu cha Stuttgart. Alipokea shahada yake ya uzamili mwaka 2010 katika Taasisi ya Teknolojia ya Karlsruhe (KIT),[3][4][5] ambapo alikuwa msaidizi wa utafiti katika Kikundi cha tafiti na Usimamizi wa Maarifa katika Taasisi ya Sayansi ya Kompyuta ya Matumizi na Lugha za Maelezo (AFIB), pamoja na Rudi Studer, kutoka mwaka 2004 hadi 2012. Mwaka 2010, alitembelea Chuo Kikuu cha Kusini mwa California (ISI).[onesha uthibitisho]

Kazi na Tafiti

hariri

Vrandečić ameshiriki katika misingi ya utoaji wa maarifa, tafiti za data, ushirikiano mkubwa kwenye mitandao, na Wavuti. Katika mwaka 2012/2013, alikuwa meneja wa mradi wa Wikidata (mradi ndugu wa Wikipedia) katika Wikimedia Ujerumani.[6] Pamoja na Markus Krötzsch (ambaye pia alikuwa KIT katika kikundi cha Usimamizi wa Maarifa), yeye ni mwendelezaji mshirika wa Semantic MediaWiki (SMW), ambayo pia ilikuwa chanzo cha msukumo wa Wikidata.[7]

Mwaka 2013, Vrandečić alifanya kazi kama mwanafalsafa wa ontolojia Google kwenye Google Knowledge Graph,[8] msingi wa uchakataji wa maarifa unaotumiwa na Google kukusanya matokeo ya injini ya utafutaji na maelezo ya kimantiki kutoka vyanzo mbalimbali.[9] Mnamo Septemba 2019, Vrandečić alitangaza kwamba anachukua jukumu jipya katika idara ya maendeleo ya Google kama Wikimedian in Residence, ambayo ilijumuisha kazi ya kuelezea miradi ya Wikimedia kwa wafanyikazi wengine.

Mnamo Julai 2020, aliondoka Google na kujiunga na Wikimedia Foundation, ambapo amehusika katika ujenzi wa Wikifunctions na Abstract Wikipedia. Inalenga kutumia data iliyopangwa kutoka Wikidata ili kuunda jukwaa la maarifa linaloendeshwa kwa lugha nyingi na mashine. Katika mchango wake wa insha katika uchapishaji wa Wikipedia wa maadhimisho ya miaka 20, Wikipedia @ 20 - Stories of an Unfinished Revolution, anafafanua hoja za kiufundi katika lugha, kubwa na hata ndogo yakiwa ndani ya matoleo ya Wikipedia.[10]

Vrandečić ni mmoja wa waanzilishi na wasimamizi wa Wikipedia ya Kikroeshia. Mnamo 2008, alihudumu kama mkuu wa programu ya kisayansi ya Wikimania. Vrandečić alihudumu katika Bodi ya Wadhamini kuanzia 2015 hadi 2016

Maisha binafsi

hariri

Vrandečić ana uraia wa Croatia na Marekani.[11] Anaishi na mkewe na binti yake katika eneo la Bay.[2]

Marejeo

hariri
  1. Hilmar Schmundt: A Wikipedia for all. How the online encyclopedia Wikipedia wants to become a universal translation machine. In: Der Spiegel. No. 3, January 16, 2021, pp. 102-103 (about Abstract Wikipedia and Denny Vrandečić)
  2. 2.0 2.1 Contributors (kwa Kiingereza). PubPub. 2020-10-15. ISBN 978-0-262-53817-6.
  3. Kigezo:Cite thesis
  4. Kigezo:DBLP
  5. "Institute AIFB - Denny Vrandecic/en". aifb.kit.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-27. Iliwekwa mnamo 2021-02-27.
  6. "Das Wikidata-Team". Wikimedia Deutschland Blog (kwa Kijerumani). 2012-04-04. Iliwekwa mnamo 2021-02-27.
  7. "Inside the Alexa-Friendly World of Wikidata". Wired (kwa American English). ISSN 1059-1028. Iliwekwa mnamo 2021-02-27.
  8. "Denny Vrandečić at Google". research.google.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-07-05.
  9. "Denny Vrandecic". The Knowledge Graph Conference (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-02-27.
  10. Vrandečić, Denny (2020-10-15). 12 Collaborating on the Sum of All Knowledge Across Languages (kwa Kiingereza). PubPub. ISBN 978-0-262-53817-6.
  11. "Eine Wikipedia für alle", Der Spiegel, Nr. 3, S. 102, 16 January 2021. 

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: