Tha De-Plow-Matz (mara nyingi hufupishwa kwa: DPT) lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lililotamba sana katika miaka ya tisini huko nchini Tanzania. Kundi linaundwa na Saigon (jina halisi Saleeh Mzee), Dolasoul (jina halisi Ahmed Dola), Trip Dogg (jina halisi Philip Mwinmanji) na Storm (jina halisi Amour Shamte). Katika familia hii kulikuwa pia na msimamizi wao aliyejulikana kwa jina la Nkwessa. Awali nyimbo zao walikuwa wanaimba Kiingereza tu. Baadaye wakawa wanaimba Kiswahili huku wakitia maneno ya Kiingereza katika mistari yao.

Tha De-Plow-Matz
Dola-Soul na Saigon
Taarifa za awali
Miaka ya kazi1992–
StudioBongo Records
MJ Records
Ameshirikiana naUnique Sisters
Wanachama wa zamani
Saigon
Dola Soul
Trip Dogg
Storm
Saigon, Dola Soul na mshirika wao.

Asili ya kundi hili lilianza katika mwaka wa 1992 pale Saigon na Tripp Dog walipokutana shule na kuanza kufanya rap kwa kujifurahisha tu. Tangu hapo vijana kadhaa walijihusisha na DPT aidha kwa muda mfupi au muda mrefu.

Katikakati mwa miaka ya 90 Saigon na Stigo wakaungana na Dola Soul ambaye alikuwa amerudi tu kutoka mjini Lagos, Nigeria, ambako huko ndiko alikokulia. Walianza kurekodi nyimbo kadhaa baadaye wakaenda studio kwa P-Funk na Master Jay, hili ilipelekea kutengenezwa albamu ya kina De-Plow-Matz. Mtindo wao na hoja zilikuwa zinaburudisha, na hivyo basi wapenzi wa mtindo huo wakaanza kuongezeka. Saigon akiwa anaenda zake nchini Uingereza mnamo 1999, na Dola anaamua kuwa msanii wa kujitegemea, kimtindo tu kundi likavunjika bila taarifa kamili ya kufa kwa kundi. Mnamo mwaka wa 2002, Saigon amerudi Tanzania, anakutana na kina Trip Dog na Dola kwa minajili ya kurudisha kundi hai lakini bila mafanikio.[1]

Baadhi ya nyimbo zao maarufu hariri

  • Turuke kwa Furaha (1996)
  • Are You Down (1999)

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Deplowmatz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.