Master Jay
Joachim Marunda Kimaryo (maarufu kama Master J; alizaliwa 9 Agosti 1973) ni muandaaji wa muziki nchini Tanzania. Ni jaji katika shindano la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki nchini maarufu kama Bongo Star Search.
Joachim Marunda Kimaryo | |
---|---|
Jina Kamili | Joachim Marunda Kimaryo |
Jina la kisanii | Rap Master Jay, Master Jay, Baba Nuru n.k. |
Nchi | Tanzania |
Alizaliwa | 9 Agosti 1973 |
Aina ya muziki | Hip Hop, Bongo Flava, Kwaya, Dansi |
Kazi yake | Mtayarishaji |
Miaka ya kazi | 1995 - sasa |
Ameshirikiana na | P Funk, Bonny Luv,Rajabu Marijani, Bizz Man, Marco Challi nk. |
Ala | Kinanda,Guitar, Kinakilishi, Kuunjini Sauti |
Kampuni | MJ Records |
Master J amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2006. Master Jay ana uwezo mkubwa sana wa utengenezaji wa muziki. Anamiliki studio tatu tofauti, moja ya muziki wa Kwaya, moja ya Bongo Flava na nyingine ya muziki wa Dansi.
Familia
haririNi mtoto wa kwanza katika familia ya Sylvan Kimaryo na Scholastica Kimaryo, ambaye alikuwa afisa wa UNDP nchini Afrika Kusini; dada yake Catherine Kimaryo anaishi nchini Tanzania akiwa mfanyabiashara mwenye kampuni yake Nchanasaa Consulting Limited (NCL).
Elimu
haririMaster J alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Upanga lakini aliishia darasa la PILI na kuhamishiwa Botswana baada ya familia yake kuhamishiwa nchini huko kikazi.
Mwaka 1996 alipata digrii ya electronics katika chuo cha City University Of London kilichopo bara Ulaya mbali na shughuli za kimuziki.
Muziki na vikwazo vya kifamilia
haririBaada ya kupata digrii yake alirudi nyumbani na kuendelea na shughuli zake za kawaida pamoja na muziki, baba yake hakutaka kabisa mwanae ajishughulishe na muziki kiasi kufikia kutaka kumuachia radhi. Pia Master Jay amefana nyimbo iitwayo anga ya mapenzi akiwa na Babbi.
Pamoja na vikwazo alivyopewa na baba yake mzazi, Master J hakuacha muziki kwa kudai kuwa umo ndani ya damu yake. Ni Jaji mkali lakini ana hekima ya Solomoni.
Studio rasmi
haririMnamo mwaka 1996 Master Jay aliamua kujishulisha kabisa na masuala ya utengezaji wa muziki kwa kuamua kuanzisha rasmi studio yake aliyoipa jina lake la "MJ Productions" japokuwa babake alikuwa haja ridhia hilo.
Baadae akatoa wimbo wa kundi la Deplowmatz, Kwanza Unit na baada ya muda kidogo tena akatoa nyimbo za kundi la 4 Crews Flavour, baada ya hapo ndipo baba yake alipoanza kuonyesha moyo na kuanza kukubali kitu anachofanya mwanaye na hii ilimpa moyo Master J wa kufanya kazi kwa bidii zaidi.
Historia
haririJoachim Marunda Kimaryo, licha ya kuwa na elimu ya juu katika uhandisi, Master Jay alikuwa na shauku kubwa ya muziki tangu utotoni, akijifunza kupiga kinanda akiwa mdogo. Baada ya kurejea Tanzania, alikabiliwa na upinzani kutoka kwa baba yake kuhusu ndoto yake ya kujihusisha na muziki. Hata hivyo, mwaka 1996 , alianzisha studio yake ya MJ Records katika kontena la futi 20 kwenye nyumba ya baba yake.
MJ Records ilichangia sana katika kukuza muziki wa Bongo Flava, ikirekodi nyimbo za wasanii na makundi mbalimbali kama Kwanza Unit, Deplowmatz, na 4 Crews Flavour. Master Jay pia alishirikiana na bendi kama Twanga Pepeta na Kwaya ya Kijitonyama katika wimbo wao maarufu "Hakuna Mungu Kama Wewe."
Mbali na kazi yake ya utayarishaji, Master Jay amekuwa jaji katika shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search, akitoa mchango mkubwa katika kugundua na kukuza vipaji vipya nchini Tanzania. Ametunukiwa Tuzo ya Muziki ya Kili mara mbili, mwaka 2004 na 2007, kuthamini mchango wake katika tasnia ya muziki.
Kwa ujumla, Master Jay anachukuliwa kama mmoja wa waanzilishi na nguzo muhimu katika maendeleo ya muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania, akileta ubunifu na weledi katika utayarishaji wa muziki.
Tanbihi
hariri
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Master Jay kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |