Djemila (kar.: جميلة "mzuri, unaopendeza") ni kijiji katika Algeria ya kaskazini penye maghofu ya Curculum (pia: Cuicul) uliokuwa mji wa Roma ya Kale katika jimbo la Numidia. Maghofu yamepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia tangu 1982.

Djemila - uwanja wa Kiroma
Djemila - uwanja wa Kiroma
Djemila - geti ya Kiroma

Curculum iliundwa mnamo mwaka 97 BK kama koloni ya Kiroma wakati wa Kaisari Nerva. Mji ulistawi vizuri hadi kuvamiwa na Wavandali 431. Baadaye ilitekwa na jeshi la Bizanti lakini iliendelea kupungua. Iliachwa tayari kabla ya kufika kwa Waarabu katika karne ya 7.

Tazama pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri